Wananchi wa mtaa wa posta kati wamemkataa afisa mtendaji wa mtaa
huo bi Esta Lwechungula kwa madai amekuwa akiwanyanyasa kwa kutumia
madaraka yake pamoja na kuwatishia kuwapeleka katika baraza la
kata pindi wanapo dai madeni yao.
Aidha wananchi hao wamesema kuwa mtendaji huyo amekuwa akiingia
mpaka chumbani wakati wa kudai michango huku akiwabambikiza kesi
ambazo si za kweli pamoja na kuwachukulia polisi wakati wa kudai
michango ambapo wametishia kufunga na kufuri ofisi ya mtaa huo
endapo halmashauri haitamuondoa mtendaji huyo.
Wamesema kuwa serikali imekuwa ikifanya makosa kuwahamisha
watendaji ambao wamefanya makosa mahala pengine na kuwapeleka
sehemu nyingine hali inayopelekea watendaji hao kuendelea kuwaibia
mali wananchi huku wakihoji fedha anazotoa kwa jeshi la polisi
linapokwenda kuwakamata anazitoa wapi ambapo wametaka kusomewa
taarifa ya mapato na matumizi juu ya fedha alizotoa kwa jeshi la
polisi hao huku wakisema amekuwa na fitina na wanachi.
Hata hivyo wamesema kuwa mtendaji huyo ameshindwa kubainisha fedha
ambazo walichangia wananchi kwaajili ya mwanafunzi ambae
walimchangia kwaajili ya kupata mahitaji mbalimbali ya shule ambapo
baada ya wananchi kutoa fedha hizo yeye alimuazima mtoto huyo hadi
sasa anashindwa kumurudishia jambo linalowakatisha tamaa wananchi.
Akizungumza mbele ya wananchi hao afisa mtendaji wa kata ya Njombe
mjini Donald Mng'ong'o amewataka wananchi kuwa na subira wakati
malalamiko yao yakifikishwa kwa mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa
Njombe na taratibu za kumuhamisha zikiendelea kufanyika ambapo
watapelekewa majibu ya kuhamishwa kwa mtendaji huyo.
Amesema kuwa wakati halmashauri ikijipanga kumuondoa mtendaji huyo
wananchi wataendelea kupata huduma za kiofisi katika ofisi hiyo
huku waliofanyiwa vibaya na mtendaji huyo wakitakiwa kupeleka
ushahidi na vielelezo ili aweze kufikishwa kwenye vyombo vya sheria
mtendaji huyo kwa sababu za msingi.
Diwani wa kata ya Njombe mjini Lupyana Fute amesema kuwa kama
malalamiko hayo ya wananchi ni ya msingi hatavumilia kuishi na
mtumishi anaejihusisha na matendo yasiyoridhisha wananchi huku
akiwataka wananchi kushiriki kikamilifu kuchyangia michango ya
ujenzi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa katika mtaa huo ikiwemo
ofisi.
Aidha bwana Fute amesema kuwa kesi zote zilizofikishwa katika
baraza la kata na mtendaji huyo zikaondolewe na waliofikishwa
kwenye baraza hilo wawe huru ili kubaini ukweli wanaolalamikia
wananchi hao.
No comments:
Post a Comment