Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Njombe bi Pindi Chana leo amekabidhi vitabu hamsini na tisa vya masomo ya sayansi katika shule ya sekondari Makambako vyenye thamani ya shilingi milioni moja ambapo pamoja na mambo mengine wanafunzi wametakiwa kujikita zaidi katika masomo ya sayansi huku wakitakiwa kuzingatia masomo wakiwa shuleni.
Akizungumza na watumishi wa halmashauri Akiwemo mkurugenzi wa halmashauri hiyo bi.Tina Sekambo,wanafunzi na walimu wa shule ya sekondari Makambako bi Chana amesema kuwa lengo la ziara hiyo ni kuwatembelea wanafunzi wa shule za sekondarimkoa wa Njombe ili kujua changamoto zinazoyakabi mazingira ya sekta ya elimu ambapo baada ya kubaini changamoto zinazoyakabili mazingira hayo atakwenda kuihamasisha serikali ili kutatua matatizo hayo.
Aidha bi.Chana amewataka wanafunzi kuepukana na mimba za utotoni na kwamba tatizo hilo limekuwa kikwazo kikubwa ambacho kimekuwa kikikwamisha maendeleo ya elimu kwa wanafunzi katika shule mbalimbali za sekondari na za msingi na kuwataka wazazi kuwa makini na kuwachukulia hatua kali wale watakaohusika kusababisha mwanafunzi kupata mimba akiwa shuleni.
Akisoma taarifa fupi mbele ya mbunge huyo mkuu wa shule ya sekondari Makambako bwana Williamu Lugurumo amesema kuwa shule hiyo imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya ukosefu wa vitabu,vyoo vya kutosha,vyomba vya madarasa 21 kwa madarasa ya kidato cha kwanza hadi cha nne na kwa madarasa ya kidato cha tano na cha sita na kwamba kuna upungufu wa vyumba vinne na ukosefu wa nyumba za walimu ikiwa zilizopo hazina hadhi nzuri zilijengwa zamani na hivyo ni chakavu.
Wakizungumza mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kukabidhiwa vitabu hivyo mkuu wa shule na wanafunzi wa shule hiyo wamepongeza kwa hatua aliyoifanya mbunge huyo na kusema kuwa hatua hiyo itasaidia kupunguza baadhi ya changamoto zinazowakabili ikiwemo ya vitabu huku akiwaomba wadau wa elimu kuendelea kutambua umuhimu wa elimu hapa nchini kwa kusaidia baadhi ya mahitaji.
Ziara ya siku mbili ya Mbunge wa viti maalum mkoa wa Njombe imelenga kuitembelea sekta ya elimu kwa mkoa wa Njombe ambapo kwa leo ameanza kwa kutembelea shule ya sekondari Makambako,shule ya sekondari Lupembe na Uwemba katika jimbo la Njombe kusini.
No comments:
Post a Comment