Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Monday, September 23, 2013

SHULE YA MSINGI MTAKATIFU BAKHITA YAFANYA MAHAFARI


















Uongozi wa Shule ya Msingi Mtakatifu Bakita Iliyopo Mjini Njombe Umeshauriwa Kutatua Changamoto Zinazoikabili Shule Hiyo Ikiwemo Upungufu wa Majengo ya Madarasa Pamoja Ujenzi wa Jiko  .

Ushauri Huo Umetolewa na Diwani wa Kata ya Uwemba Edward Mwalongo
Ambaye Alikuwa Mgeni Rasmi Katika Mahafali ya Kwanza ya Darasa la Saba Kwa Shule Hiyo na Kusema Kuwa Changamoto Hizo Zinaweza Kutatuliwa na Uongozi wa Shule Kwa Kushirikiana na Wazazi.

Katika  Risala Iliyosomwa na Wanafunzi Wanaohitimu Elimu ya Msingi wa Shule ya Mtakatifu Bakita Imebainisha Changamoto Mbalimbali Ikiwemo Ukosefu wa Maktaba  , Bwalo la Chakula  , Uhaba wa Vifaa Huku Wakipendekeza Kutatuliwa Kwa Changamoto Huizo.

Katika Mahafali Hayo Zaidi ya Shilingi Laki Mbili Zimepatika Kwa Ajili ya Ujenzi wa Jiko , Fedha Ambazo Zitatumika Katika Ununuzi wa Saluji na Mchanga Huku Mgeni Rasmi Akiahidi Kuchangia Tofali Elfu Kumi.

Jumla ya Wanafunzi Arobaini na Nne Wamehitimu Darasa la Saba Kwa Mwaka 2013 Katika  Shule Hiyo

No comments:

Post a Comment