Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Tuesday, September 24, 2013

WANANCHI WA KATA YA NJOMBE MJINI WALALAMIKIA KUWEPO KWA UCHAFU KATIKA KITUO CHA AFYA NJOMBE MJINI NA WAUUGUZI KUTOKUWEPO KITUONI WAKATI WA USIKU







 DIWANI KATA YA NJOMBE MJINI LUPYANA FUTE AKIWA KWENYE MKUTANO WA HADHARA KATIKA MTAA WA KWIVAHA NA MITAA MINGINE YA KATA YA NJOMBE MBJINI IKIWEMO MTAA WA POSTA KATI KERO NI KITUO CHA AFYA NJOMBE MJINI WAHUDUMU HUWA WANAKUWA HAWAPO NYAKATI ZA USIKU



 WANANCHI WA MTAA WA KWIVAHA WAKIWA KWENYE MKUTANO WA HADHARA ULIOFANYIKA KATIKA OFISI YA MTAA HUO





Diwani wa Kata ya Njombe Mjini Lupyana Fute Hii Leo Ametembelea Kituo Cha Afya cha Njombe Mjini na Kujionea Uchafu  Uliopo Katika Kituo Hicho Yakiwemo Maji Machafu Yanayotiririka na Mlundikano wa Taka Huku Akimwagiza Afisa Afya wa Halmashauri ya Mji Kuhakikisha Mazingira ya Kituo Hicho Yanakuwa Safi.

Ziara Hiyo ya Diwani Fute Imekuja Ikiwa ni Siku Moja Baada ya Wananchi wa Mtaa wa Kwivaha Kulalamikia Kitendo cha Kukamatwa na Maafisa Afya Kwa Kosa la Kutofanya Usafi Ili Hali Kituo Hicho cha Afya ni Kichafu na Hakuna Hatua Zozote za Kisheria Zinazochukuliwa Dhidi ya Uongozi wa Kituo Hicho.

Hapo jana Katika Mkutano wa Hadhara Baina ya Diwani Fute na Wakazi wa Mtaa wa Kwivaha Walilamikia Masuala Mbalimbali Yanayofanywa na Baadhi ya Viongozi wa Mtaa na Serikali Ikiwemo Huduma Mbovu Inayotolewa Katika Kituo cha Afya cha Njombe Mjini,  Utozwaji Kodi Pamoja na Kuchangishwa Michango Pasipo Kupewa Stakabadhi.

Akitolea Ufafanuzi Baadhi ya Hoja Zilizotolewa na Wakazi wa Mtaa wa Kwivaha Kwenye Mkutano Huo wakati alipo tembelewa na diwani wa kata ya Njombe mjini hapo jana, Afisa Afya wa Halmashauri ya Mji Njombe  Bonface Msemwa Amekiri Kuwepo Kwa Baadhi ya Hoja Zilizotolewa  na Wakazi Hao Likiwemo Suala la Uchafu  Katika Kituo Hicho Huku Akiahidi Kulifanyia Kazi Haraka Iwezekanavyo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa kwivaha bwana Maxona Nathanael amesema lengo la mkutano huo lilikuwa ni kumtambulisha afisa mtendaji aliyehamia kwenye mtaa huo,utaratibu wa ugawaji wa pembejeo za ruzuku kwa mwaka huu pamoja na kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wananchi Na kupewa elimu juu ya sheria ya uzoaji taka.

No comments:

Post a Comment