ZAIDI YA WAFANYABISHARA
400 KUTOKA NCHI SITA ZIKIWEMO ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI NA KUSINI MWA
AFRIKA SADC WATASHIRIKI KATIKA MAONESHO YA KIMAITAFA YA BIASHARA
YATAKAYOFANYIKA NOVEMBA MWAKA HUU JIJINI MBEYA.
MWENYEKITI WA CHAMA CHA
WAFANYABIASHARA WENYE VIWANDA NA KILIMO TCCIA MKOANI MBEYA BWANA LWITIKO
MWAKALUKWA AKIZUNGUMA NA WAANDISHI WA HABARI MKOANI MBEYA AMESEMA LENGO
MAONESHO HAYO NI KUWAPA FURSA WAFANYABISHARA WADOGO NA WAKATI KUKUZA BISHARA ZAO
NA KUTANGAZA FURSA ZA UTALII ZILIZOPO UKANDA WA KUSINI MWA TANZANIA.
BWANA MWAKALUKWA AMESEMA
KUWA MAONESHO HAYO AMBAYO YANADHAMINIWA NA TCCIA KWA KUSHIRIKINA NA WADAU
WENGINE YATAFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA JOHN MWAKANGALE JIJINI MBEYA AMBAPO
WAJASIRIAMALI NA WANANCHI WA MIKOA YA NYANDA ZA JUU KUSINI WATAJIFUNZA NAMNA YA
KUFUNGASHA BIDHAA ZAO KUTOKA KWA WAFANYABIASHARA WENGINE WA WANACHI ZITAKAZO
SHIRIKI AMBAZO NI TANZANIA, KENYA, ZIMBABWE,MALAWI, ZAMBIA NA JAMHURI YA
KIDEMOKRASIA YA CONGO (DRC).
NAYE AFISA MTENDAJI WA TCCIA MBEYA BI. ADELINA MUNAZI AMESEMA KUWA
KUPITIA MAONESHO HAYO WANACHAMA WA TCCIA NA WANACHI WATAPATA FURSA YA KUTANDAA
KIBIASHARA NA KUWATAKA WAYATUMIE VIZURI KWA MANUFAA YAO NA TAIFA KWA UJUMLA.
|
No comments:
Post a Comment