Thursday, September 5, 2013
JESHI LA POLISI KITENGO CHA USALAMA BARABARANI MKOA WA NJOMBE LA AANZA KUKABILIANA NA AJALI ZA BARABARANI
Kufuatia Ongezeko la Matukio ya Ajali za Barabarani Katika Siku za Hivi Karibuni Mkoani Njombe,Jeshi la Polisi Mkoani Hapa Limeanza Kuchukua Hatua za Haraka Ili Kuweza Kukabiliana na Matukio Hayo Ambayo Pamoja na Mambo Mengine Yamekuwa Yakisababisha Vifo Kwa Wananchi.
Miongoni Mwa Hatua Hizo ni Pamoja na Kufanya Mikutano ya Hadhara na Kuzungumza na Wananchi Pamoja na Madereva wa Pikipiki za Kubeba Abiria Maarufu Kama Bodaboda Mjini Njombe.
Akiwa Katika Mkutano na Wananchi na Madereva Hao Katika Mtaa wa Kambarage Mjini Njombe Kamanda wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Mkoa wa Njombe Maro Chacha Anatumia Fursa Hiyo na Kuwaelimisha Madereva na Wananchi Hao Juu ya Namna ya Uendeshaji Salama na Kuzingatia Sheria za Usalama Barabarani.
Anasema Kwa Kutambua Tatizo Kubwa Linalowakabili Madereva Hao la Kutokuwa na Mafunzo Stahiki ya Uendeshaji Salama, Jeshi Hilo Liko Tayari Kuwaandalia Mpango Maalum Utakaoratibiwa na Jeshi la Polisi Kwa Kushirikiana na Wataalamu wa Mafunzo ya Udereva Kutoka Chuo Cha VETA Songea, na Kuhakikisha Kila Dereva Anapata Mafunzo Rasmi Yatakayosaidia Kupunguza Tatizo Hilo.
Anasema Pamoja na Mambo Mengine Wanatarajia Kuanza Kutoa Mafunzo ya Usalama Barabarani Kila Siku za Ijumaa Kwa Madereva Hao, na Kusema Kuwa Hali Hiyo Itasaidia Kupunguza Kama Sio Kumaliza Kabisa Tatizo la Ajali za Barabarani Mkoani Njombe Kwa Kuanzia na Mtaa wa Kambarage.
Pankras Matinya ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Kambarage Anapongeza Hatua Zilizoanza Kuchukuliwa na Jeshi la Polisi Katika Kukabiliana na Matukio Hayo na Kusema Wao Kama Serikali ya Mtaa, Hawako Tayari Kuona Matukio ya Ajali za Pikipiki Yakiendelea Kujitokeza Kwenye Mtaa Huo.
Kwa Upande Wao Baadhi ya Madereva Walioshiriki Mkutano Huo Wamelipongeza Jeshi la Polisi Kwa Hatua Walizoanza Kuzichukua za Kukabiliana na Matukio Hayo na Kuahidi Mbele ya Kamanda Kuwa Hawatomvumilia Dereva Yoyote Atakaevunja Sheria.
Hii Inakuja Ikiwa ni Siku Chache Tangu Kutokea Kwa Ajali Mbaya ya Pikikipi Katika Mtaa wa Kambarage Mjini Njombe na Kusababisha Kifo Cha Dereva wa Pikipiki Hiyo Baada ya Kupasuka Vibaya Sehemu za Kichwani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment