Friday, September 20, 2013
CHAMA CHA MAPINDUZI CHAIAGIZA HALMASHAURI YA MJI KUTOLEA UFAFANUZI JUU YA TARATIBU ZA KUWAHAMISHA WATENDAJI BILA KUKABIDHI MALI ZA VIJIJI
Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Njombe Kiumeutaka Uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Kutolelea Ufafanuzi Kuhusu Utaratibu wa Kuwahamisha Watendaji wa Vijiji na Kata Wanaodaiwa Kuondoka na Mali za Ofisi Pamoja Fedha za Michango ya Wananchi Kwa Ajili ya Shughuli za Miradi ya Maendeleo.
Aidha Chama Hicho Pia Kimeitaka Halmashauri Hiyo Kupeleka Mhandisi wa Ujenzi Kwa Ajili ya Kufanya Usanifu wa Ujenzi wa Bweni la Shule ya Sekondari ya Anna Makinda Ili Kunusuru Vifaa Vya Ujenzi Vilivyonunuliwa Kwa Lengo la Ujenzi wa Bweni Hilo
Akiongea Kwenye Kikao cha Ndani cha Wajumbe CCM na Wataalam wa Serikali wa Kata ya Ihanga Alipokuwa Katika Ziara ya Siku Moja Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Njombe Adam Msigwa Amesema Amekuwa Akisikia Malalamiko Mengi Kutoka Kwa Wananchi Juu ya Watendaji wa Vijiji Kuhamishwa Bila Kukabidhi Mali za Ofisi Vikiwemo Vitabu Vya Stakabadhi Pamoja na Fedha Zilizochangwa na Wananchi Kwa Ajili ya Miradi ya Maendeleo
Mwenyekiti Huyo wa CCM Wilaya Ameutaka Uongozi wa Halmashauri Hiyo ya Mji wa Njombe Kushughulikia Malalamiko ya Wananchi Hao Ili Kujenga Imani Kwa Wananchi Wanaowaongoza.
Kwa Upande Wake Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Edward Mwalongo Ambaye Pia ni Diwani wa Kata ya Ameahidi Kuyafuatilia Malalamiko ya Wananchi Hao na Kuwabaini Watendaji Waliohamishwa Bila Kukabidhi Mali za Ofisi na Michango ya Wananchi.
Awali Wakizungumza Mbele ya Viongozi wa CCM Wilaya ya Njombe Baadhi ya Wajumbe na Wataalam wa Kata Hiyo Wamesema Kufuatia Watendaji Hao Kuondoka na Mali za Ofisi Wananchi Wamekuwa Wagumu Katika Kuchangia Miradi ya Maendeleo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment