Mwanafunzi
Ajuaye Ngeve mhitimu wa darasa la saba shule ya Msingi Nyamihuu
akikabidhiwa cheti chake na mgeni wa heshima katika mahafali ya 34 ya
shule hiyo Bw Jackson Kiswaga leo
MWENYEKITI wa
Halmashauri ya wilaya ya Iringa na diwani wa kata ya Nzihi jimbo la
Kalenga Bw Stivin Mhapa amempongeza mkazi wa kijiji cha Nyamihuu
anayeishi jijini Dar es Salaam Bw Jackson Kiswaga kwa ahadi yake ya
kujitolea kusomesha sekondari wanafunzi watatu wa shule hiyo
ambao watafanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa Taifa wa Darasa
la saba mwaka 2013 na kushindwa ada ya kwenda Sekondari.
Mhapa
ametoa pongezi hizo leo katika mahafali ya 34 ya shule ya
Msingi Nyamihuu mara baada ya Bw Kiswaga kutoa hutuba yake na
kuahidi kusomesha wanafunzi hao .
Alisema kuwa kilichofanya na
Kiswaga ni mfano wa kuigwa na wengine na kuwataka wazazi
kuhakikisha wanawasimamia vema watoto wao ili kuendelea na masomo
zaidi.
Pia Mhapa alitaka msaada huo kusimamiwa vizuri na
viongozi wa kijiji na kuwa wale watakaochaguliwa kunufaika na
msaada huo ni vema majina yao yakatangazwa katika mkutano wa hadhara
ili kila mwananchi aweze kujua na kama kuna uchakachuaji basi
kufahamika.
Kwani alisema baadhi ya watu wamekuwa si
waaminifu na kuwaacha walengwa na kuwapa nafasi wenye uwezo badala
ya wale wasio na uwezo.
Kwa upande wake Kiswaga alisema
mbali ya ahadi hiyo pia ataichangia shule hiyo kiasi cha Tsh 500,000
kwa ajili ya kuchangia ununuzi wa madawati katika shule hiyo. |
No comments:
Post a Comment