Diwani wa kata ya Mfriga akipokea pia vifaa vya michezo kwaajiliya vijana wa kata hiyo.
Katibu mwenezi wa ccm mkoa wa Njombe Honoratus Mgaya akiwa ameongozana na Mbunge wa Njombe Kaskazini.
Diwani Wa kata ya Lupembe Bi wapalila akipokea vifaa vya michezo kwaajili ya vijana wa kata yake.
Wananchi wa kata ya mjimwema Makambako wamelalamikia kukosa huduma za uhakika za matibabu katika kituo cha afya kinachotarajiwa kupandishwa hadhi na kuwa hospitali ya Halmashauri ya Makambako ambapo wagonjwa wamekuwa wakiandikiwa dawa na kwenda kununua madukani.
Wakiongea katika ziara ya Mbunge wa Njombe kaskazini bwana Deo Sanga ya kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi wamesema kuwa wanashangazwa kuona kituo cha afya Makambako kimekuwa kikikosa huduma za dawa hata panadol hali inayowaweka katika wakati mgumu wananchi hao.
Katika hatua nyingine wananchi hao wameilalamikia halmashauri ya Makambako kwa kupima viwanja vya kujenga kwenye vyanzo vya maji huku wakiitaka halmashauri hiyo kuweka mipango miji kwa kuzingatia mahitaji ya wananchi ikiwemo kuweka maeneo ya shule,zahanati na viwanja vya michezo.
Mbunge wa jimbo la Njombe kaskazini Deo Sanga amesema kama halmashauri imeruhusu kujengwa kwa nyumba mpaka kwenye vyanzo vya maji inakwenda kinyume na sheria ya mazingira ambapo amesema inatakiwa halmashauri kupitia wakuu wa idara inatakiwa kuondoa bikoni za viwanja zilizopo mpaka kwenye vyanzo vya maji ili kutunza mazingira na vyanzo hivyo huku kwa upande wa afya akisema huduma zitapatikana vizuri kituo hicho kitakapopandishwa hadhi.
Frola Mdugo ni kaimu Mganga mkuu wa kituo cha afya Makambako amekili kukosekana kwa dawa katika kituo hicho na kusema kuwa hali hiyo inasababishwa na kuwepo kwa ongezeko kubwa la watu pamoja na serikali kupeleka dawa chache ambazo imedaiwa zinakwisha baada ya wiki moja tangu kupelekwa jambo ambalo huwalazimu kuwaandikia dawa wagonjwa na kuruhusu kwenda kununua kwenye maduka ya madawa.
Kwa upande wake kaimu afisa ardhi na maliasili wa halmashauri ya Makambako amesema bwana Nail Mbyopyo amesema hana uhakika kwamba kuna viwanja vimepimwa mpaka kwenye vyanzo vya maji na kusema kuwa halmashauri itakwenda kutembelea maeneo hayo na kuyafanyia marekebisho ikiwemo kuwaondoa wale nwaliojenga mpaka kwenye vyanzo vya maji.
Ziara ya Mbunge huyo imelenga kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa na wananchi ambapo kwa siku ya leo ameweza kutembelea madarasa manne ambayo anayajenga kwa nguvu zake ikiwemo madarasa mawili katika shule ya msingi Magegele na madarasa mawili katika shule ya sekondari mpya ya Mashujaa ambayo anatarajia kukabidhi mwishoni mwa mwaka huu.
No comments:
Post a Comment