Meneja
wa uwanja wa John Mwakangale wa maonesho ya Nanenane Kasilati Mwakibete
akiwa katika ziara ya kuangalia maandalizi ya Nanenane
Waandishi wakiwa kwenye Ziara
Shughuli Mbalimbali zikiendelea
Mkaguzi
msaidizi wa Magereza Daniel Wabare ambaye pia ni msimamizi wa Banda
la Magereza Nane nane akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari.
Hatimaye maandalizi ya maonesho
ya sikukuu ya Wakulima Nanenane Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yatakayofanyika
katika Viwanja vya John Mwakangale Uyole Mkoani Mbeya yamekamilika kwa asilimia
Miamoja.
Akizungumzia hali ya maandalizi
ya maonesho hayo kwa Mwaka 2013, Meneja wa Uwanja huo Mwakibete Kasilati
amesema hadi sasa baadhi ya Washiriki wameshaanza kufanya shughuli zao kama
kawaida.
Amesema Mwaka huu kunahamasa kubwa sana tofauti na miaka ya
nyuma ambapo Wafanyabiashara wengi wamejitokeza hivyo kuenea uwanja mzima
mapema.
Amesema kuna maeneo ambayo
hayakuwahi kutumika kutokana na baadhi ya washiriki kujikusanya sehemu moja
ambapo ameongeza kuwa safari hii hali hiyo haitakuwepo baada ya kutawanyika
kila upande.
Aidha baadhi ya mabanda
yaliyotembelewa yalionekana kuendelea na shughuli zao ikiwa ni pamoja na
kufanya usafi, kuboresha bustani na ukarabati mdogodogo.
Mabanda yaliyotembelewa na
kutia hamasa kwa washiriki wa Mwaka huu ni pamoja na ujenzi wa sehemu ya
kuoneshea Wanyama hai ambao ni Simba, Chui, Mbega, Kobe na wengine kibao.
Mabanda mengine yanayoendelea
na kazi ni pamoja na banda la Jeshi la Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa(JKT)
huku baadhi ya vibanda vya Chakula (mama ntilie) na grosari zikiendelea na
shughuli zao.
Maeneo Mbalimbali
Mmoja wa waandishi akiwa anapiga picha mambo mbalimbali
No comments:
Post a Comment