Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Tuesday, July 16, 2013

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 16. 07. 2013.

chanzo Mbeya yetu blog

[ DIWANI  ATHUMANI   - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

WILAYA YA MBARALI - AJALI YA  PIKIPIKI  KUGONGA GARI NA KUSABABISHA KIFO
 MNAMO TAREHE 15/07/2013 MAJIRA YA SAA 16:15HRS HUKO MWAMBEGELE BARABARA YA MBEYA/IRINGA WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. GARI NO .T605 AJP/T.693 AKE AIN YA SCANIA LIKIENDESHWA NA DEREVA MOSHI S/O MZEE, MIAKA 42, MUHA, MKAZI WA IRINGA LILIGONGWA NA PIKIPIKI ISIYOFAHAMIKA NA KUSABABISHA KIFO KWA ABIRIA WA PIKIPIKI AITWAYE SIKUJUA  D/O DAUDI, MIAKA 30, MSAFWA NA MKAZI WA MAJENJE IGURUSI.  MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA DAKTARI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. CHANZO CHA AJALI HIYO NI MWENDO KASI WA PIKIPIKI NA KUSHINDWA KUIMUDU KISHA KULIVAMIA GARI HILO KWA NYUMA.  GARI LIPO KITUO CHA POLISI IGURUSI. DEREVA WA PIKIPIKI ALIKIMBIA NA PIKIPIKI MARA BAADA YA AJALI HIYO JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI  DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO DEREVA ALIYESABABISHA AJALI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAKE ZICHUKULIWE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MARA MOJA.
WILAYA YA MOMBA  - AJALI YA MOTO NA KUSABABISHA KIFO.
NAMO TAREHE 14/07/2013 MAJIRA YA SAA 06:00HRS HUKO KIJIJI CHA KAPELE KATA YA KATELE WILAYAYA MOMBA MKOA MBEYA. MTOTO AITWAYW BRANDINA D/O ALINJITA, MIAKA 3,  MNYAMWANGA ALIFARIKI DUNIA BAADA YA  KUUNGUA MOTO SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE  BAADA YA  KIBANDA KILICHOJENGWA KWA NYASI KUUNGUA MOTO WAKATI AKIWA NDANI NA WAZAZI WAKE WAKIWA SHAMBANI WAKIVUNA MAHARAGE. CHANZO CHA MOTO HUO NI KIBERITI ALICHOKIWASHA MTOTO HUYO. TAARIFA KITUONI TAREHE 15/07/2013 MAJIRA YA SAA 19:15 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA WAZAZI NA WAZEZI KUWA MAKINI NA KUTOWAACHA WATOTO WADOGO NYUMBANI BILA UANGALIZI ILI KUWEZA KUEPUSHA MADHARA YANAYOWEZA KUTOKEA.
WILAYA YA MBEYA - KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.
MNAMO TAREHE 15/07/2013 MAJIRA YA SAA 09:0HRS HUKO UYOLE JIJINI MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA/MISAKO  WALIWAKAMATA MALUKUSI S/O DEMSI, MIAKA 21, AKIWA NA WENZAKE SITA WOTE RAIA WA ETHIOPIA  WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI [.] WATUHUMIWA WAPO MAHABUSU TARATIBU ZA KUWAKABIDHI IDARA HUSIKA ZINAENDELEA.  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA JUU YA MTU/WATU WANAOWATILIA SHAKA ILI HATUA DHIDI YAO ZICHUKULIWE HARAKA IKIWA NI PAMOJA NA RAIA WA KIGENI.
[ DIWANI  ATHUMANI   - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments:

Post a Comment