Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Tuesday, July 16, 2013

MBUNGE WA JIMBO LA NJOMBE KASKAZINI AENDELEA NA ZIARA YAKE YA SIKU 26 LEO KATIKA VIJIJI VYA ILENGITITU,MADUMA NA IBUMILA KWA KUCHANGIA UJENZI WA MIRADI NA KUKAGUA..




 Wanafunzi wa shule ya msingi Ilengititu wakiiimba nyimbo mbele ya Mbunge huyo

 Wataalamu mbalimbali wa halmashauri ya wilaya ya Njombe
 Katibu mwenezi wa ccm mkoa wa Njombe Honoratus pilimini Mgaya akizungumza na wananchi




 Joyce Mwakalukwa  afisa maendeleo ya jamii wa halmashauri ya wilaya ya Njombe akijibu swali la kuwasaidia walemavu wa vijijini lililoulizwa  na wananchi wa kijiji cha Ilengititu



 Mbunge wa jimbo la Njombe ksakazini Deo Sanga akikagua miradi mbalimbali na hapa ni zahanati ya kijiji cha Ibumila






 Mbunge akiwa katika shule ya sekondari ya J.M Makweta akikagua na kuongea na wanafunzi pamoja na walimu


 Shule ya msingi Maduma ambapo mkutano ulifanyikia
 Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Njombe bwana Filbert Mbwilo



 Mbunge wa jimbo la Njombe kaskazini Deo Sanga akikagua ujenzi wa nyumba ya mganga wa zahanati ya Ibumila kijijini humo





Afisa mtendaji wa kijiji cha Ibumila akisoma taarifa fupi mbele ya Mbunge huyo
Wananchi wa kijiji cha Ilengititu kata ya Kichiwa wilayani Njombe wametakiwa kutambua umuhimu wa kupeleka watoto wao kujiunga na masomo ya sekondari pindi wanapofaulu ikiwa ni pamoja na kuendelea kuchangia chakula shuleni ili kuongeza idadi ya ufaulu kwa wanafunzi.

Akizungumza mara baada ya hotuba ya Mbunge wa jimbo la Njombe kaskazini Deo Sanga mkuu wa shule ya msingi Ilengititu bwana Lusungu Myale amesema shule hiyo kwa mwakajana ilifanikiwa kufaulisha wanafunzi 44 kati ya wanafunzi 50 ambapo kati yao wanafunzi kumi hawakupelekwa kujiunga na masomo ya sekondari huku wanafunzi wanne wakiacha kuendelea na masomo kutokana na sababu mbalimbali.

Aidha bwana Myale amesema shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa vitabu 1500 vya kiada,walimu watatu,vyoo matundu 8,madawati 55 pamoja na madarasa mawili na ukosefu wa huduma za maji.

Katika taarifa fupi iliyosomwa na Afisa mtendaji wa kijiji cha Ilengititu bwana Phanuel Myamba kwa Mbunge wa jimbo hilo bwana Deo Sanga ameiomba serikali kusaidia kusogeza huduma za maji katika shule hiyo ili kuepukana na matukio yanaoweza kujitokeza ya ubakaji kwa wanafunzi huku akisema kijiji hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ujenzi wa ofisi ya kijiji,saruji mifuko 50.

Amesema kuwa kijiji hicho kimeibua mipango mikakati ya kuanzisha miradi mbalimbali itakayoanza kutekelezwa kwa mwaka 2013/2014 ikiwemo kutekeleza mradi wa maji tatizo linalowakabili wananchi na shule na taasisi ,ujenzi wa zahanati,ofisi ya kijiji,ujenzi wa vyoo na madarasa katika shule ya msingi Ilengititu.

Emmanuel Mayemba ni kaimu afisa elimu wa shule za msingi amesema kuwa vitabu vipo ofisi za halmashuri ya wilaya hivyo watavipeleka katika shule hiyo huku akisema tatizo la upungufu wa walimu ni tatizo linalozikabili halmashauri mbalimbali kwa mkoa wa Njombe kwa kukosa watumishi na kusema kuwa halmashauri itakapokuwa imepata walimu hao watapelekewa.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Njombe kaskazini amewataka wananchi kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi huku akiwahamasisha kwa kuchangia mifuko 50 ya saruji katika kijiji cha Ilengititu ambapo katika kijiji cha Maduma ameahidi kupeleka saruji mifuko hamsini pamoja na kijiji cha Ibumila akiahidi kuchangia bati 34 za nyumba ya mganga wa zaanati ya kijiji hicho huku saruji akisema atawasiriana na halmashauri ya wilaya ili kusaidia mifuko iyo.



Wakulima wa zao la mahindi na viazi kata ya Kichiwa na mtwango  wilayani  Njombe wapo hatarini kukumbwa na janga la njaa endapo wataalamu wa kilimo watashindwa kudhibiti wadudu waharibifu ambao wameibuka mwaka huu na kuharibu mazao yanayostawishwa mashambani msimu wa masika.

Akisoma Risala fupi mbele ya Mbunge wa jimbo la Njombe kaskazini Deo Sanga ,Afisa mtendaji wa kijiji cha Ibumila bwana Erasto Kapinga amesema tatizo hilo limekuwa likiwapa mashaka mkubwa wakulima wa kijiji hicho ambapo wataalamu wa kilimo na mifugo walizipata taarifa za kuwepo kwa wadudu hao lakini hakuna kinachoendelea juu ya wadudu hao.

Akijibu malalamiko ya wananchi juu ya wadudu waharibifu kaimu afisa ardhi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe bwana ..Amesema kwa halmashauri ya wilaya ya Njombe tatizo hilo haliwezi kutatuliwa ambapo halmashauri kupitia wataalamu wa kilimo walikwisha chukua hatua za kupeleka kwa wataalamu wa kituo cha utafiti wa magonjwa ya mimea Uyole Mbeya na Soko Inne ambapo bado hawajapatiwa majibu.

Aidha afisa huyo bwana ....amekili kuwepo kwa wadudu wanaosababisha uharibifu wa mazao ya mahindi na viazi na kusema kuwa tatizo hilo limeenea na maeneo jirani na kijiji hicho ya Mtwango ambapo amesema wananchi wanatakiwa wakiwaona wanatakiwa kuuwa haraka pamoja na kufuga kuku kwa wingi wakufuga huria ili waweze kuwashambulia wadudu hao .

Amesema kuwa kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa kupelekea kuwepo kwa wadudu hao ambapo jitihada za serikali zinaendelea ili kufanikisha tatizo hilo kwa wakulima wa vijiji ambavyo ugonjwa huo umeibuka.
Kwa Upande wake Mbunge wa Njombe kaskazini Deo Sanga amesema halmashauri inatakiwa kurifuatilia kwa haraka tatizo hilo ili kuwaondoa hofu wananchi wa kata hizo juu ya kilimo kwa mwaka huu.

No comments:

Post a Comment