Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Wednesday, July 17, 2013

MBUNGE WA JIMBO LA NJOMBE KASKAZINI LEO AMEENDELEA TENA NA ZIARA YAKE KATIKA KATA YA MTWANGO VIJIJI VYA ITUNDUMA NA ILUNDA KATA YA MTWANGO PAMOJA NA KIJIJI CHA IKANDO KATA YA KICHIWA..

 KATIBU MWENEZI WA CCM MKOA WA NJOMBE HONORATUS MGAYA AKIWAMBIA WANANCHI KWAMBA CCM SIYO MBAYA ILA BAADHI YA VIONGOZI WALIOKO MADARAKANI WALIOCHAGULIWA KUPITIA CCM NI WABAYA.
 wananchi wa kijiji cha Ikando wakisilikiza hotuba ya Mbunge wao Deo Sanga leo
 VIFAA VYA MICHEZO AKIKABIDHI KWA VIJANA WA TIMU ZA MPIRA WA MIGUU KATIKA KIJIJI CHA IKANDO






 HAPA ALIKUWA KUTEMBELEA MIRADI INAYOTEKELEZWA NA WANANCHI WA KIJIJI CHA ITUNDUMA NA HAPA NI SHULE YA MSINGI ITUNDUMA B AKIWA NA KATIBU WAKE VASCO MGUNDA NA WATAALAMU WENGINE WA HALMASHAURI YA WAILAYA YA NJOMBE.

 BAADA YA KUFIKA OFISI YA KIJIJI CHA ITUNDUMA MBUNGE DEO SANGA NA WATAALAMU WA HALMASHAURI



 HII NI KWAYA YA KIJIJI CHA ITUNDUMA BAADA YA KUWASILI MBUNGE HUYO WAKAIMBA NYIMBO ZA KUMPONGEZA NA MAOMBI MBALIMBALI







 HAPA NDIYO OFISI YA KIJIJI CHA ITUNDUMA KATA YA MTWANGO WILAYA YA NJOMBE NA HAWA NI WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI ITUNDUMA


 AFISA MTENDAJI WA KIJIJI CHA ITUNDUMA AKISOMA TAARIFA FUPI KWA MBUNGE



 MENEJA WA SHIRIKA LA NISHATI YA UMEME NCHINI TANESCO WILAYA YA NJOMBE OMARY ALLY AKIJIBU MASWALI YALIOULIZWA NA WANANCHI JUU YA UMEME

 KATIBU MWENEZI WA CCM MKOA WA NJOMBE HONORATUS MGAYA


 DIWANI WA KATA YA MTWANGO AMBAE PIA NI MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE VALENCE KABELEGE AKITOLEA MAJIBU JUU YA MATUMIZI YA SOKO AMBALO LIMETELEKEZWA BILA KUTUMIWA NA WAFANYA BIASHARA KATIKA KATA YA MTWANGO



 KWA MAKINI WANANCHI WA KIJIJI CHA ITUNDUMA KATA YA MTWANGO WILAYANI NJOMBE WAKISUBIRI KITAKACHOZUNGUMZWA NA MBUNGE WAO DEO SANGA



 KAIMU AFISA KILIMO NA MIFUGO WA HALMASHAURI YA WILAYA PASIFIKI MHAPA AKITOLEA MAELEZO NAMNA YA KUWASAIDIA WANANCHI JUU YA WADUDU WAHARIBIFU WA MAZAO NA MATUMIZI YA PEMBEJEO AINA YA MINJINGU AMBAYO INALALAMIKIWA NA WANANCHI WENGI MKOA WA NJOMBE KUWA HAIFAI



 ITUNDUMA WAKITAWANYIKA BAADA YA MKUTANO KUAHIRISHWA





 HAWAO NI WANAKWAYA WA KIJIJI CHA ILUNDA WAKIWAKILISHA WANANCHI KWA KUIMBA
 PALIKUWA HAPATOSHI KWA MAPOKEO NA MAANDALIZI MAKUBWA YA KUMPOKEA MBUNGE WAO







HAPA MBUNGE HUYO AKIWA KATIKA KIJIJI CHA ILUNDA NA HUKO NDIKO ALIKOMALIZIA MKUTANO KWA SIKU YA LEO
Wananchi wa kata za kichiwa na Mtwango wilayani Njombe wametakiwa kuitumia vizuri miradi wanayosaidiwa na mashirika mbalimbali yasiyo  ya kiserikali ili kuinua uchumi wa wananchi na serikali ambapo kwa kufanya hivyo itasaidia kuondoa utegemezi na kupunguza baadhi ya changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili.

Akizungumza na wananchi katika mikutano ya vijiji vya Ikando,Itunduma na Ilunda Mbunge wa Jimbo la Njombe kaskazini Deo Sanga ameyapongeza mashirika hayo kwa moyo huo wa kujitolea ambapo pamoja na mambo mengine amesema hilo ni jambo la kuyapongeza na kuwataka waendelee kuibua miradi mingine kwa kushirikiana na serikali za maeneo wanapoishi.

Katika hatua nyingine bwana Sanga ameipongeza serikali kwa kuweka viunganishi vya miundombinu inayopitika kwa wananchi wilayani Njombe ambapo amewataka baadhi ya wananchi ambao bado wanakabiliwa na changamoto za kutopitika kwa miundombinu hiyo kuwa wavumilivu wakati serikali ikiendelea kujipanga kuboresha maeneo hayo.

Ameendelea kuhimiza ulinzi na usalama katika mali zao na kusema kuwa waharifu wa mali mbalimbali wanatoka miongoni mwao wenyewe wananchi na kuwataka kuwataja kutoa taarifa kwa uongozi wao ama kituo cha polisi ili hatua kali zichukuliwe dhidi yao huku akiwataka viongozi kwa kushilikiana na jeshi la polisi kutumia njia ya kupiga kura katika kuwabaini waharifu katika maeneo ya wananchi.

Akisoma taarifa fupi ya kijiji cha Itunduma afisa mtendaji wa kijiji hicho bwana Godfrey Kiowi amesema kuwa wananchi wamepongeza mashirika yasiyo ya kiserikali kwa ushiriki wao mkubwa wa kusaidia ujenzi wa miradi ikiwemo mradi wa mbuzi na kuku kutoka shirika la PADI,shirika la NADO kwa kutoa elimu ya mashamba darasa kuwajengea uwezo wakulima juu ya mbinu bora za kilimo na mashirika ya wahisani ya KTFKTF na Acra kwa misaada mbalimbali.


Akiwa katika kijiji cha Ilunda Bwana Sanga ameahidi kupeleka bati hamsini kwaajili ya ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi Ilunda ili kuhamasisha maendeleo kwa wananchi.

Kuhusu tatizo la wadudu waharibifu limeendelea kuwa tishio kwa kata hiyo ya Mtwango ambapo kila Mbunge huyo anapopita suali kubwa ni namna ya kuwaangamiza wadudu waharibifu wa mazao ya mahindi na viazi pamoja na matumizi ya pembejeo aina ya minjingu.


Ambapo Wakulima wa Mazao ya Mahindi na Viazi wa Kata za Mtwango na Kichiwa Wameiomba Serikali Kuwasadia Kukabiliana na Wadudu Waharibifu Wanaoshambulia Mazao na Kutishia Kuibuka Kwa  Tatizo la Chakula Katika Vijiji Hivyo.

Katika Risala Iliyosomwa na Erasto Kapinga Wakati wa Ziara ya Mbunge wa Jimbo la Njombe kaskazini Deo Sanga Imeeleza Kuwa Katika Msimu wa Kilimo Uliopita Kumeibuka Wadudu Waharibifu Ambao Wameshambulia Mazao Katika Vijiji Vya Kata Hizo.

Aidha Wananchi Hao Wamesema Tayari Wametoa Taarifa Kwa Wataalam wa Kilimo na Mifugo Wilaya ya Njombe Juu ya Kuwepo Kwa Tatizo Hilo Lakini Hadi Hivi Sasa Hakuna Jitihada Zozote Zilizochukuliwa.

Akijibu Malalamiko ya Wananchi Hao Kaimu Afisa Kilimo Halmashauri ya Wilaya ya Njombe  Pasific Mhapa Amekiri Kuwepo Kwa Tatizo la Wadudu Waharibifu wa Mazao na Kwamba Serikali Inafanya Jitihada za Kukabiliana na Wadudu Hao.

Amesema Idara ya Kilimo na Mifugo imepeleka Wataalam wa Mifugo na Kilimo Pamoja na Sampuli  ya Wadudu Hao Katika Vituo Vya Utafiti wa Magonjwa ya Mimea Vya Uyole Mbeya na Sokoine Mkoani Morogoro Kwa Ajili ya Utambuzi wa Wadaudu Hao.

Katika Hatua Nyingine Bwana Mhapa Amewashauri Wakulima wa Maeneo Hayo Kufuga Kuku Kwa Mtindo wa Ufugaji Huria Ili Kukabiliana na Wadudu Hao Kama Njia ya Awali Wakati Serikali Ikilitafutia Ufumbuzi Tatizo Hilo.

No comments:

Post a Comment