Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Sunday, July 14, 2013

MBUNGE WA NJOMBE NKASKAZINI AITAKA HALMASHAURI YA MAKAMBAKO KUWEKA VIPIMO STAHILI VYA KUPIMIA NYANYA ZA WAKULIMA KULIKO ILIVYO SASA NYANYA ZINAPIMWA KWA MTINDO WA LUMBESA

Mbunge wa Jimbo la Njombe Kaskazini Deo Sanga Ameiagiza Halmashauri ya Mji wa Makambako Kuhakikisha Inamaliza Migogoro Mbalimbali ya Wananchi , Ukiwemo Mgogoro wa Ardhi Kati ya Wananchi wa Kijiji cha Usetule na Ofisi ya Kata ya Mahongore.

Akizungumza Katika Muendelezo wa Ziara Yake ya Kutembelea na Kukagua Shughuli za Maendeleo Katika Jimbo Lake , Katika Kata ya Mahongore Bwana Sanga Amesema Migogoro Mingi ya Ardhi Inayojitokeza Inachangiwa na Baadhi ya Wananchi Kutokuwa na Uelewa wa Kutosha Juu Hati Miliki ya Ardhi na Kuutaka Uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Makambako Kutoa Elimu Kwa Wananchi.

Aidha Bwana Sanga Pia Ameitaka Halmashauri Hiyo Kuhakikisha Mazao ya Wakulima Yanauzwa Kwa Vipimo Stahili Pamoja na Kudhibiti  Ununuzi wa Mazao Kwa Mtindo wa Lumbesa Unaofanywa na Baadhi ya Wafanyabiashara Ama Madalali wa Mazao.

Ameongeza Kuwa  Halmashauri Kupitia Idara ya Biashara Inatakiwa Kuwahamasisha Wanunuzi wa Mazao Kwenda Kununua Mazao Hayo Kwenye Masoko Yaliyoko Maeneo ya Vijijini Jambo Ambalo Litasaidia Kumaliza Tatizo la Ununuzi wa Mazao Kwa Mtindo wa Lumbesa na Kumnufaisha Mkulima .


Wakiongea Mbele ya Mbunge Huyo wa Jimbo la Njombe Kaskazini Wananchi wa Kijiji cha Usetule  Wamelalamikia Kuwepo Kwa Migogoro ya Ardhi , Ununuzi wa Mazao Kwa Mtindo wa Lumbesa Pamoja na Baadhi ya Maduka  ya Pembejeo za Kilimo Kuuza Mbegu Zilizochini ya Kiwango, Ukosefu wa Huduma ya Umeme na Miundombinu Mibovu ya Barabara.

No comments:

Post a Comment