HAPA MBUNGE HUYO ANAKABIDHI JEZ NA MPIRA KWA VIJANA TAGAMENDA
HAWA NI WANANCHI WA KIJIJI CHA TAGAMENDA WAKICHEZA NGOMA MBELE YA MBUNGE
SHULE YA MSINGI TAGAMENDA
MKUTANO WA MWISHO ULIMAZIKIA KATIKA KIJIJI CHA ITIPINGI KATA YA IGONGORO
KAIMU AFISA KILIMO NA MIFUGO BRAITON MLIVATWA AKIELEZEA JUU YA MBOLEA AINA YA MINJINGU
KAIMU MKRUGENZI BWANA MBWIROAKIHAMASISHA VIONGOZI WA VIJIJI KUWEKA MASANDUKU YA MAONI
WATAALAMU WENGINE WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE AKIWEMO KAIMU MUHANDISI WA UJNZI BWANA CHARLES MBIDUKA
KATIBU MWENEZI CCM WA MKOA WA NJOMBE HONORATUS MGAYA
BAADA YA MKUTANO KUMALIZIKA WANANCHI HAPA WANATAWANYIKA
Serikali Wilayani Njombe Kupitia Idara ya Kilimo
Imetakiwa Kuongeza Mashamba Darasa Kwa Ajili ya Kuwaonesha Mfano Kwa Wananchi
na Wakulima Juu ya Matumizi ya Mbolea za Minjingu Ili Kuwajengea Imani Wakulima
Hao na Kuendelea Kuitumia Mbolea Hiyo.
Kauli Hiyo Imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Njombe
Kaskazini Bwana Deo Sanga Kufatia Malalamiko ya Baadhi ya Wakulima Juu ya
Ubaora wa Mbolea Aina ya Minjingu Wakati
Akiongea na Wananchi wa Kata ya Igongoro Katika Ziara Yake , Ambapo Amewataka Wakulima na Wananchi
Kuondoa Hofu Juu ya Mbolea Hiyo na Badala Yake Wawatumia Maafisa Ugani Waliopo
Katika Vijiji Vyao.
Aidha Bwana Sanga Amewataka Wataalam wa Kilimo na Mifugo
Kuwatembelea Wakulima Mara Kwa Maa Ili Kubaini Matatizo Yanayowakabili Katika
Shughuli Zao za Kilimo na Ufugaji
Akijibu Baadhi ya Maswali na Malalmiko ya Wanachi Juu ya
Mbolea ya Minjingu Kaimu Afisa Kilimo na Mifugo wa Halmashauri ya Wilaya ya
Njombe Bryton Mlivatwa Amesema Mbolea Hiyo Inahitaji Maji Mengi Hivyo Katika
Maeneo Ambayo Hayana Maji ya Kutosha Inaonekana Haifai na Kwamba Serikali
Haiwezi Kutoa Mbolea Ambazo Hazijafanyiwa Utafiti wa Kina.
Amesema Mbolea ya Minjingu Inavirubisho Vingi Ambayo
Vinatija Kwa Mazao Mbalimbali na Kuongeza Kuwa Halmashauri Hiyo Tayari
Imeanzisha Mashamba Darasa Kwa Baadhi ya Kata na Kuwataka Wananchi Kwenda
Kujifunza Namna ya Kuitumia Mbolea Hiyo Huku Akisema Kuwa Baadhi ya Maeneo
Wamenufuika na Mbolea ya Minjingu.
Akielezea Kuhusu Ujenzi wa Miundombinu ya Barabara Maeneo
ya Vijijini Kaimu Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Charles
Mbiduka Amesema Serikali Bado Inaendelea Kuboresha Barabara za Kata na Kuongeza
Kuwa Makalavati Yatawekwa Kwenye Barabara Hizo Kwani Kwa Sasa Walikua Wanajenga
Madaraja.
Awali Wakitoa Kero Zao Mbele ya Mbunge wa Jimbo la Njombe
kaskazini Wakati wa Ziara Katika Kijiji cha Itipingi Wananchi Hao Walilalamikia
Masuala Mbalimbali Ukiwemo Ubovu wa Miundombinu ya Barabara na Ubora wa Mbolea ya Minjingu.
Katika hatua nyingine wananchi hao wameendelea kulalamikia kilo cha vipimo vya mazao vinavyotumika kupimia nyanya katika soko kuu la nyanya Makambako na kuitaka serikali iwazuie wafanyabiashara wanaonunua zao la nyanya kwa mkulima na kupimia vipimo vinavyowaridhisha wakulima na kwamba wanapimia matenga hali inayomkandamiza mkulima.
Ziara hiyo kesho inaendelea katika taarafa ya Lupembe ikiwa kwa makambako amekwisha kumaliza kwa kutembelea vijiji na kata kukagua maendeleo na utekelezaji wa miradi yao.
No comments:
Post a Comment