Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Monday, July 22, 2013

MBUNGE WA JIMBO LA NJOMBE KASKAZINI JANA AMEFUNGUA JENGO LA OFISI YA KIJIJI CHA IYEMBELA KATA YA MATEMBWE TAARAFA YA LUPEMBE

Mbunge wa jimbo la Njombe kaskazini Bwana Deo Sanga leo amezindua jengo la ofisi katika kijiji cha Iyembela kata ya Matembwe lenye zaidi ya shilingi milioni 22 ambapo pamoja na mambo mengine amewataka wananchi kuendelea kuwa na mshikamano katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya vijiji ili kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili.

Akizungumza na wananchi mara baada ya ufunguzi huo bwana Sanga amesema kutokana na kukamilisha ujenzi wa jengo la ofisi hiyo wananchi wanatakiwa kuanza kufikiria ujenzi wa zahanati ya kijiji ili kupunguza gharama za kusafiri umbali mrefu hali inayopelekea baadhi ya akina mama wajawazito kujifungulia njiani jambo ambalo ni kinyume na sheria.

Aidha bwana Sanga ameahidi kufikisha nguzo za umeme ambazo wananchi wameomba kuongezewa ili wananchi wote waweze kupata huduma za miundombinu ya umeme.

Katika hatua nyingine bwana Sanga amewataka viongozi wa vijiji na kata katika taarafa ya Lupembe kutatua matatizo yanayowakabili wananchi kwa baadhi ya maeneo ikiwemo migogoro ya ardhi ambayo imeonekana kujitokeza kwa wingi hasa katika vijiji vya kata za kidegembye na Matembwe na baadhi ya maeneo mengine.

Akisoma taarifa fupi ya kijiji cha Iyembela afisa mtendaji wa kijiji hicho bi.Furaha Manwingi amesema kuwa pamoja na kufanikiwa kujenga ofisi hiyo lakini pia wamefanikiwa kupanda ekari 22 za miti,kutengeneza madawati 38 pamoja na ukarabati wa shule ya msingi Iyembela ambao umegarimu shilingi milioni moja na laki nne.

Bi.Manwingi amesema kuwa kijiji hicho kinakabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo kukosa namba ya usajili,maji ya bomba huku wakiomba pembejeo za kilimo kufika kwa wakati ili kufanikisha sekta ya kilimo katika kijiji hicho.

Kwa upande wao wananchi wakiuliza maswali kwa mbunge huyo wamelalamikia kiwanda cha chai Lupembe na kwamba wamiliki wa kiwanda hicho wamevamia mashamba ya wananchi na kwamba wanashindwa kuelewa  serikali kuruhusu viwanda vya chai kujengwa na mmiliki mmoja jambo linalosababisha wakulima wa chai kukosa uhuru wa kufanya biashara ya chai Lupembe.

No comments:

Post a Comment