Mkuu wa shule ya msingi Lyalolo kata ya Matembwe bwana Christopha Mgunda ameyaomba mashirika mbalimbali mkoani Njombe kutembelea maeneo ya vijijini kutoa misaada kwa watoto yatima na wasiyojiweza ili kusaidia watoto hao kupata fursa ya kuendelea na masomo kama watoto wengine.
Akiongea na Uplands fm mapema leo bwana Mgunda amesema kuwa shule ya msingi Lyalalo inajumla ya watoto yatima 25 ambapo pamoja na mambo mengine watoto hao wamekuwa wakisoma katika mazingira magumu kutokana na kukosa mahitaji ya msingi ikiwemo mavazi na chakula.
Aidha mkuu huyo wa shule bwana Mgunda amesema mbali na hayo wananchi pia wanaowajibu wa kuwasaidia watoto hao kwa kushirikiana na serikali za vijiji ili kulijenga taifa la kesho.
Kuhusu utoaji chakula shuleni amesema chakula kimekuwa kikitolewa kila siku za masomo licha yakuwepo kwa baadhi ya wazazi ambao hawatambuai umuhimu wa kupatiwa chakula shuleni na kuwataka viongozi wa serikali za vijiji kuendelea kutoa elimu kuhusiana na chakula.
Kwa upande wao wazazi wa kijiji cha Lyalalo wamesema sababu inayopelekea baadhi kushindwa kuchangia chakula shuleni ni kutokana na kukosa uwezo wa kifedha na chakula kwakuwa uwezo wao ni mdogo kwani baadhi ya watoto wanaishi na bibi na babu zao kutokana na kuwa yatima.
Kaimu Afisa elimu shule za msingi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe bwana Emmanuel Mayemba amese ni vema wazazi wakahamasika kuchangia chakula shuleni na kwamba hali hiyo inasaidia kukuza kiwango cha taaluma kwa wanafunzi.
No comments:
Post a Comment