Wednesday, July 24, 2013
WANANCHI ISOLIWAYA WA WASHTAKI VIONGOZI MBALIMBALI AKIWEMO DIWANI WA VITI MAALUMU WA TAARAFA YA LUPEMBE KWA KUSHINDWA KUWATEMBELEA MPAKA ZIARA YA MBUNGE NDIPO WANATEMBELEA
Wananchi wa kijiji cha Isoliwaya wilayani Njombe wamelalamikia kuwepo kwa viongozi ambao hawapendi kutembelea wananchi na kusikiliza matatizo yanayo wakabili wakiwemo madiwani wa viti maalumu wa chama cha mapunduzi pamoja na viongozi wengine ambapo pamoja na mambo mengine wameomba kutembelewa mara kwa mara ili kusikiliza kero mbalimbali zilizopo.
Wakitoa malalamiko hayo kwa Mbunge wa jimbo la Njombe kaskazini bwana Deo Sanga alipotembelea kijiji hicho wamesema tangu kutangazwa kwa wananchi kwa viongozi mbalimbali hawajawahi tembelewa na kujua matatizo yao hali inayopelekea migogoro mingi kutokea kutokana na kuwepo kwa viongozi wazembe kutembelea kusikiliza kero zao na kutoa ushauri.
Katika hatua nyingine wananchi hao wameendelea kulalamikia wamiliki wa kiwanda cha chai Lupembe kwa kufika kuchukua majani ya chai wakati wa usiku hali inayohatarisha usalama wa wakulima wa kurudi nyumbani na kwamba chai wanayochuma mashambani imekuwa ikichukuliwa kuanzia majira ya saa tatu mpaka saa tano usiku huku akina mama wakiacha watoto wao nyumbani peke yao wakisubiri kuuza majani hayo ya chai jambo ambalo mbunge huyo amesema atalifuatilia kwa wahusika wa chai hiyo.
Akijibu swali lililoulizwa na wananchi hao diwani wa viti maalumu wa taarafa ya Lupembe bi Frolintina Mwenda amemesema kuwa yeye hahusiki na kata ya Matembwe na kwamba yeye yupo kata mbili ambazo walitengewa kusimamia za Kidegembye na Lupembe barazani huku akisema aliyepangiwa kusimamia kata hiyo alifariki dunia na kuteuliwa mmoja wa kusimamia kata hoyo na hivyo kuahidi kufikisha taarifa hizo ili aweze kuwafikia wananchi hao.
Kumekuwa na tatizo la baadhi ya viongozi kushindwa kuwatembelea wananchi vijijini na kusikiliza matatizo yao ambapo pamoja na mambo mengine wananchi wanalazimika kutumia jitihada zao kusuruhisha matatizo yaliopo miongoini mwao ambapo migogoro mbalimbali imekuwa ikitokea kwa kukosa ushauri toka kwa viongozi wao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment