Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Friday, July 19, 2013

SHULE YA MSINGINGI LOLE INATARAJIWA KUVUNJWA MADARASA YAKE ILI KUJENGA UPYA KWA MTINDO WA KISASA KWANI YALIOPO NI CHAKAVU

 WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI LOLE KATA YA IKUNA
 MBUNGE WA JIMBO LA NJOMBE KASKAZINI DEO SANGA AKIZUNGUMZA NA BAADHI YA WAZAZI JUU YA UCHAKAVU HUO




 TANGU SHULE HIYO IJENGWE MWAKA 1978 TENA CHINI YA KIWANGO BADO INADUMU MPAKA SASA WALIMU WALALAMIKIA SERIKALI JUU YA MAJENGO HAYO KUWA YANAWAKATISHA TAMAA YA KUENDELEA KUFUNDISHA


 MBUNGE DEO SANGA MAARUFU KWA JINA LA PA PEOPLE AKISALIMIANA NA WANAFUNZI WA SHULE HIYO






















 HAPA WALEMAVU WA KIJIJI CHA IKUNA WANAONESHA KIPAJI CHAO CHA KUIMBA MBELE YA MBUNGE DEO SANGA

 WALEMAVU WA VIUNGO MBALIMBALI WA KATA YA IKUNA KIJIJI CHA IKUNA WILAYANI NJOMBE



 HAPA NI KIJIJI CHA NYOMBO KATA YA IKUNA AKAPOKELEWA KWA SHANGWE NA NDEREMO










Serikali imekusudia kuvunja madarasa yote ya shule ya msingi lole katika kata ya Ikuna wilayani Njombe kutokana na kuwepo kwa uchakavu uliokithili kwenye madarasa shuleni hapo ambapo pamoja na mambo mengine Mbunge wa jimbo la Njombe kaskazini Deo Sanga ameahidi kupeleka bati hamsini na gari la kusombea tofari ili kujenga madarasa ya kisasa.

Katika ujenzi huo halmashauri ya wilaya ya Njombe imeahidi kuchangia milioni kumi na moja ili kufanikisha ujenzi huo huku wananchi wakishiriki kufyatua tofari na kusogeza mawe ujenzi unaotarajiwa kuanza mwezi wa nane na yanatarajiwa kukamilishwa mwishoni mwa mwaka huu ifikapo Mwezi wa kumi na moja na kumi na mbili.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Lole Mbunge wa jimbo la Njombe kaskazini Deo Sanga amesema kuwa pamoja na kuwa kijiji hicho kinakabiiwa na ujenzi wa madarasa ya kisasa katika shule ya msingi Lole lakini ameitaka halmashauri kupeleka huduma za maji katika kijiji hicho kutokana na wanafunzi na wananchi kukosa kabisa huduma ya maji huku wanafunzi wakifuata huduma hiyo mbali kwa matumizi ya shuleni.

Amesema kuwa kwa sasa ziara yake inalenga kuwatembelea wananchi wa vijiji ambavyo mwezi april hakufanikiwa kuvifikia akiwa na ujumbe wa kutoka Bungeni juu ya bajeti iliyoongezwa bungeni na kusema kuwa sekta iliyo ongezewa bajeti kubwa ni sekta ya madini.

Valentino Hongory ni diwani wa kata ya Ikuna amemshukuru mbunge huyo kwa kuchangia  ujenzi  wa miradi mbalimbali na kusema kuwa kwa kijiji cha Ikuna kinakabiliwa na tatizo la ujenzi wa kituo cha afya  ili kuwarahisishia huduma za matibabu akina mama wajawazito na wagonjwa wengine wa kata hiyo na kata jirani na kusema pia wanaujenzi wa nyumba za walimu katika shule ya msingi Ikuna na sekondari.

Akizungumzia kufikishwa kwa huduma za maji katika kijiji cha Lole kaimu Muhandis wa halmashauri ya Wilaya ya Njombe bi Zaina Issa amesema kuwa kwa mwaka huu kijiji hicho hakipo kwenye bajeti ambapo ameutaka uongozi wa kijiji na kata kuandika maombi na kupeleka halmashauri ya wilaya ili bajeti ya kipindi kinachofuata waweze kuingiza kwenye bajeti na hatimae kupelekewa maji ambapo kwa kijiji cha Ikuna amesema tatizo la maji linasababishwa na baadhi ya wananchi wanaojenga kwenye vyanzo vya maji na kuwataka wananchi hao kutunza vyanzo vya maji.

Amesema halmashauri imetafuta chanzo kingine kitakacho hudumia vijiji mbalimbali vya Ibumila,Ikuna na vijiji vingine vya jirani.


Akisoma taarifa fupi ya maendeleo ya kijiji cha Lole kwa niaba ya afisa mtendaji wa kijiji hicho mwalimu wa shule ya msingi Lole bwana Bahati Kaminyoge amesema kijiji hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uchakavu wa madarasa ya shule ya msingi Lole,ukosefu wa samani za shule zote mbili lole na Idongela,tatizo la maji na ujenzi wa nyumba mbili za walimu na kukosa huduma za afya.

Katika ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi Lole wananchi wanatakiwa kuchangia elfu ishilini kwa kila mmoja ambapo ziara ya Mbunge huyo hapo kesho itaendelea katika kata ya Igongoro vijiji vya .

No comments:

Post a Comment