Sunday, May 5, 2013
WASANII CHIPUKIZI WA MUZIKI, FILAMU NA NGOMBA ZA ASILI WATARAJIA KUNUFAIKA KWA KUREKODIWA KAZI ZAO BURE BAADA YA KUPAMBANISHWA MEI 8 KATIKA TAMASHA LITAKALOFANYIKA MJINI NJOMBE.
MWENYEKITI CHADEMA JIMBO LA NJOMBE KUSINI ALLY MUHAGAMA AKIANGALIA SHOW ZA VIJANA KWA NIA YA KUWAWEZESHA WAWEZE KUREKODI KAZI ZAO.
KATIBU WAKE OBADIA CHOGA MWENYE KOFIA MEZANI HAPA
Kwenye meza alioko katikati ni mwenyekiti wa CHADEMA jimbo la Njombe kusini Ally Muhagama maaru kwa jina la Sagasaga.
B. Alon akiwa na wenzake katika ukumbi wa Vegas akifanya maonesho siku ya uundwaji wa makundi ya muziki.
.
Vijana wakionesha uwezo wao na vipaji katika muziki kwa kucheza kwa stepu mbele ya mgeni rasmi HAPATA TOSHA SIKU YA MCHUJO NA MAJAJI KUFANYA KAZI ZAO ZA KUWAPATA WASANII WATAKAO WAKILISHA MKOA WA NJOMBE KIBURUDANI
MWENYEKITI CHA CHADEMA JIMBO LA NJOMBE KUSINI ALLY MUHAGAMA {maarufu Sagasaga} Akiwa kwenye picha ya pamoja na wasanii hao. Picha na Elia Kayombo.
Wasanii Mkoani Njombe Wametakiwa kuhepuka kujihusisha na mambo ya kisiasa na badala yake wakijikite katika kutoa kazi zao za muziki zenye mafundisho na kuionya jamii juu ya matukio maovu yakiwemo mauaji,ubakajina ujambazi hapa nchini.
Akizungumza na wasanii wa Filamu,Bongo Flavour na Sanaa Mbalimbali katika ukumbi wa Vegas jana mwenyekiti wa CHADEMA jimbo la Njombe kusini Ally Muhagama Maarufu Kama Dokta Sagasaga amesema endapo wasanii wataachana na mambo ya siasa na kutoa mafundisho juu ya kuhepuka maovu itapelekea nchi ya Tanzania kuendelea kudumisha amani na utulivu na kazi zao zitakuwa zenye tija kwa jamii.
Akizzungumza kwa upande wake katibu wa CHADEMA jimbo la Njombe kusini Obadia Choga amesema lengo la kuunda makundi ya wasanii mbalimbali mkoani Njombe ni kutaka kuinua vipaji mbalimbali vya wasanii wa Njombe kwa wasanii hao kushirikiana kwa pamoja pasipo kuibiana kazi zao na kutunga nyimbo zenye mafundisho kwa jamii kuliko kuimba nyimbo za kimapenzi pekee.
Wakizungumza mara baada ya kuhitimisha zoezi la uundwaji wa makundi ya wasanii mbalimbali wasanii wa muziki wa bongofraver na sanaa za filamu Mjini Njombe wamesema endapo Chama hicho kitawasaidia wasanii wenye uwezo mkubwa wa kuimba na kuigiza itakuwa imewasaidia kwa kiasi kikubwa kwani nao watakuwa miongoni mwa wasanii maarufu hapa nchini.
Wamepongeza pia kwa hatua ya CHAMA hicho kuibua wazo la kuwaunganisha wasanii hao na kusema kuwa wanaomba kiwasaidia hadi mwisho ili wasanii wa Njombe nao waweze kuwakilisha mkoa wa Njombe katika taifa la Tanzania na Mataifa kwa ujumla badala ya kuendelea kuwaita wasanii wa Dar pekee ikiwa hata Njombe wapo.
Jumla ya makundi manne ya wasanii hao yameundwa jana ambayo yatakwenda kupambanishwa tarehe nane mwezi mei mwaka huu katika ukumbi wa Vegasi kwa majaji kuwapata wasanii bora ambapo katika shindano hilo mshindi wa kundi la kwanza atarekodiwa nyimbo zake bure za audio na video ikiwa ni pamoja na filamu nao kundi la kwanza litareakaodiwa filama ambayo wataendelea kuiuza wasanii wenyewe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment