UMASKINI, shida na
matatizo ya usafiri katika ziwa nyasa, barabara ya lami kutoka njombe hadi
manda na ucheleweshwaji wa ujenzi wa chuo cha veta, ndivyo vinavyomkosesha
amani na kumnyima uzingizi mbunge wa Ludewa katika mkoa wa njombe Deo
Filikunjombe imefahamika.
Akizungumza na kipindi
hiki Filikunjombe alisema pamoja na baadhi ya wenzake kutokumwelewa kufuatia
misimamo yake hajutii wala kubadili msimamo wake na kwamba yeye hawezi kuumizwa
na mambo ya kitaifa wakati wananchi wa Ludewa wakiendelea kuteseka kwa kukosa
mahitaji muhimu ambayo kimsingi ni haki yao haiingii akilini hata kidogo. Aling’aka
‘’’ Serikali isipo
badilika mimi na wananchi wa Ludewa tupo tayari kuandamana tukiwa tumevalia
mashati ya kijani na suruali nyeusi mpaka kieleweke.’’ Kauli ya
filikunjombe
Filikunjombe
aliyataja mambo matatu yanayomuumiza na kumnyima usingizi na kupelekea kusimama
akiwa na nguvu bila hofu bungeni kuwa ni pamoja na usafiri wa meli mpya katika ziwa nyasa ambayo
ni ahadi ya rais pamoja na ukarabati wa meli mbili zilizopo ambazo ni chakavu,
kuharakishwa kwa barabara ya lami kutoka njombe hadi manda na kuharakishwa kwa
ujenzi wa chuo cha Veta ili wananchi wake wafaidi matunda ya miaka 50 ya uhuru
wa nchi hii.
Wananchi wa kata ya
Lumbila wao wanafuata huduma ya afya wilayani kyela mkoani mbeya ambako hutumia
mitumbwi kusafirisha wagonjwa na wajawazito.’’’’ Alisema mzee Joseph
Mwakasungura
DEO
alikataa kuunga mkono hoja ya waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania
katika bunge la bajeti kwa kusema serikali siyo sikivu katika mambo ya
utekelezaji hasa inapobainika katika baadhi ya mambo yanayokwenda kinyume na
matokeo kuwa mabaya haichukui hatua kwa viongozi na watendaji husika.
Alisema
viongozi wamekuwa Wakiendelea kulindana wao kwa wao kana kwamba hawaoni
kinachofanyika mbele yao yapo mengi nitaeleza machache kwa muda huu elimu
katika nchi hii pamoja na kwamba tumejenga shule nyingi za sekondari kila kata.
‘’’’’
mwaka 2012 kulikuwa na ongezeko la ufaulu wa wanafunzi wa Darasa la Saba
kujiunga kidato cha kwanza tukajipongeza sana kwa matokeo hayo lakini
ikagundulika ufauru huo ni pamoja na watoto wasiojua kusoma na kuandika zaidi
ya elfu kumina moja na waziri mkuu akaunda tume lakini hadi sasa hatujaona
kuwajibika kwa yeyote katika wizara husika,
‘’’’tena
imekuwa vivyo hivyo 2013-kufeli kwa wanafunzi kidato cha nne vibaya zaidi pia
tume imeundwa kuchunguza na tunajua haitakuwa na lolote zaidi ya Funika
kombe Mwanaharamu apite.’’’’ Alisema kwa masikitiko filikunjombe
Kauli
hiyo Ikimaanisha tusahau mambo ya tumeiliopita tujadili ya sasa
hukutunajua hakuna kitakacho fanyika kiutekelezaji, aidha alisema tukumbuke
Filikunjombe
alisema elimu ya msingi itolewayo katika nchi hii sio bure tena
kama tunavyosema bali ina gharama zinazotokana na michango mingi
inayomghalimu mzazi kwa mtindo wa michango inayojumlisha kuanzia
Tsh,6000/= mpaka 12,000/= kwa mwanafunzi mmoja kwa mwaka na kwamba ni heri
turudishe ada wazazi wajiandae.
Deo
alionesha kushangazwa na Serikali hii ilivyokaa kimya huku ikijua
wananchi wanaona haya yote yanayofanyika na kwakupitia matatizo haya
pesa ya umma inatumika vibaya tena akastaajabu kuona wabunge
wenzake wakigeuka kupinga kila hoja za wapinzani bila kuchunguza zinahusu nini
kwa maslahi ya wananchi.
mwisho
No comments:
Post a Comment