Friday, May 31, 2013
JESHI LA POLISI MKOA WA NJOMBE LA WAKUTANISHA VIONGOZI WA DINI KUTOKA WILAYA MBILI KUTATHIMINI JUU YA ULINZI NA USALAMA.
MKUU WA UPELELEZI MKOA WA NJOMBE
KAMANDA WA POLISI MKOA WA NJOMBE FULGENCE NGONYANI
Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe wakitoka kwenye kikao na viongozi wa dini,Na Michael Ngilangwa.
Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Limewataka Viongozi wa Dini Kuendelea Kudumisha Amani na Utulivu na Kukemea Migogoro ya Kidini Katika Nyumba za Ibada Pamoja na Kuwataja Watu Wanaochochea Chuki za Kidini Miongoni Mwa Watanzania.
Aidha Jeshi Hilo Pia Limewataka Waumini Kuacha Kujihusisha na Mambo ya Kisiasa Katika Masuala ya Kidini Kwani Kwa Kufanya Hivyo Itazidi Kuchochea Machafuko ya Kidini Jambo Linaloweza Kuhatarisha Amani ya Nchi na Utulivu Uliopo.
Akizungumza na Viongozi wa Dini Mjini Njombe Kamanda wa Polisi Mkoani Njombe Fulgency Ngonyani Amesema Lengo la Kuwakutanisha Viongozi Hao ni Kwaajili ya Kutambua Nafasi ya Viongozi wa Dini Katika Kutunza na Kulinda Amani ya Nchi.
Amesema Viongozi wa Dini Wana Nafasi Kubwa Katika Kuelimisha Waumini na Jamii Kuhusu Athari na Namna ya Kuhepuka Migogoro ya Kidini na Mivutano ya Kisiasa na Kusema Kuwa Ushirikiano Kati ya Jeshi la Polisi na Viongozi Hao ni Nguzo Imara Katika Kukabiliana na Migogoro Hiyo.
Aidha Kamanda Ngonyani Pia Amekemea Tabia ya Baadhi ya Askari Wanaotoa Taarifa za Siri Juu ya Taarifa za Uhalifu Zinazowasilishwa Kwa Jeshi Hilo Kutoka Kwa Raia Wema
Wakizungumza Kwenye Mkutano Huo Baadhi ya Viongozi wa Dini Waliohudhuria Mkutano Huo Wameliomba Jeshi la Polisi Kuchukua Hatua Dhidi ya Matukio ya Uhalifu na Ubakaji Yanayojitokeza Kwasasa Mkoani Hapa
Kwa upande Wake mrakibu msaidizi wa polisi Focas Malengo na maafisa upelelezi mkoa wa Njombe wakasemaushirikiano ni wa muhimu katika jamii ikiwemo kutoa taarifa za uharifu iwe kwa vikosi vya jeshi la polisi ama mwananchi yeyote anaekwenda kinyume na matakwa ya umma pamoja na kuwataja wale wote wanaohusika kukosesha jamii kwa kuwaibia,mauaji,ubakaji na udokozi.
Mkutano Huo Ulilenga Kuzungumzia Namna ya Ushiriki wa Viongozi wa Dini Katika Kutunza na Kulinda Amani Iliopo Kwasasa Hapa Nchini Ambayo Imeanza Kutetereka Kutokana na Kuanza Kujitokeza Kwa Itikadi za Kidini Miongoni Mwa Watanzania.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment