Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Njombe ambae pia ni Mbunge
wa jimbo la Njombe kaskazin Deo Sanga (kushoto) akiwa na katibu mkuu
wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana mara baada ya kuwasili viwanja vya
polisi Makambako kwa ajili ya kuhitimisha ziara yake mkoa wa Njombe leo.Na Francis Godwin.
....
Mbunge wa jimbo la Njombe Kaskazin Deo
Sanga ameitata serikali kuwachukulia hatua kali madaktari wa
hospitali na zahanati za umma wanaouza dawa badala ya kutoa bure kwa
wagonjwa wanaofika kupatiwa matibabu katika Hospitali hizo za umma.
Sanga ambae ni mwenyekiti wa chama
cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Njombe ametoa kauli hiyo leo katika
uwanja wa Polisi Makambako mbele ya katibu mkuu wa CCM Taifa Ndugu
Abdalrahman Kinana wakati akieleza changamoto mbali mbali
zinazowakaba wananchi wa jimbo lake hasa katika sekta hiyo ya afya.
Sanga alisema kuwa mbali ya serikali
ya CCM kuendelea kutekeleza ilani ya chama hicho kwa kasi kubwa ila kwa upande
wa idara ya afya mbali ya serikali kuendelea kuboresha sekta hiyo ila
bado changamoto kubwa ni hujuma zinazofanywa na madaktari hao kwa
kuuza dawa za umma katika maduka yao.
" Tunapenda kuipongeza sana serikali
yetu ya CCM chini ya Rais Dkt Jakata Mrisho Kikwete kwa kazi kubwa
inayoendelea kufanya katika kuwatumikia wananchi ....ila naomba leo
kusema tena hapa kama nilivyopata kusema bungeni kuwa serikali
imekuwa ikitoa dawa bila kuangalia ongezeko kubwa la wananchi katika
maeneo hayo kwani mbali ya wananchi kuongezeka ila kiwango cha dawa
kinachotolewa ni kile kile cha miaka 10 iliyopita na mbaya zaidi dawa
hizo zinahujumiwa kwa kuuzwa katika maduka ya madaktari na wauguzi"
Mbunge huyo alitaka kuwekwe
utaratibu wa serikali kuwabana wanaouza madawa ya umma katika maduka
yao ikiwa ni pamoja na kutaifisha dawa hizo kwa maslahi ya umma.
Katika hatu nyingine Sanga alisema
kuwa mbali ya kutekeleza ilani ya CCM katika jimbo hilo kwa fedha za
umma ila kupitia kampuni yake ya Jah People ameendelea kufanya mambo
makubwa katika jimbo hilo ikiwa ni pamoja na kata ya ya mlowa ambayo
ameanza kujenga madarasa matatu wakati Itandililo
tumeweza kupeleka mabati 180 huku shule ya msingi Magegele tumeanza
ujenzi wa shule ya msingi kwa madarasa mawili.
Pia katika eneo la Ninga amekabidhi
msaada wa mabati 120kwa ajili ya sekondari mpya pia zipo Zahanati
mbali mbali kwa kupeleka mashuka ,mablanketi na mambo mengine mengi
ikiwa ni pamoja na kuanza kuweka lami katika barabara za mji wa
Makambako ambazo zilikuwa ni kero kubwa
Hata hivyo mbunge huyo amemwomba
msaada wa bati 600 na saruji mifuko 200 katibu mkuu kwa ajili ya
kusaidia ujenzi wa miradi mbali mbali ya maendeleo katika jimbo hilo
ombi ambalo limekubaliwa na katibu huyo ikiwa ni pamoja na kuahidi
kuchangia kikundi cha wajasilia mali Makambako kiasi cha Tsh milioni
10 |
No comments:
Post a Comment