Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Tuesday, April 23, 2013

KANISA LA TAG NJOMBE LIMELAANI MAVAZI YANAYOTUMIWA KINYUME NA MAADILI,VYOMBO HUSIKA NA WANANCHI WATAKIWA KUKEMEA MAVAZI YA HOVYO KAMA NGUO FUPI KWA WANAWAKE NA WANAUMEKUVALIWA HADHARANI



 SHATI LA NJANO NI MCHUNGAJI WA KANISA LA PENTEKOST MKOA WA MBEYA BENJAMINI KIVOVELE NA SUTI NYEUSI MCH.CEFENIA TWEVE WAKITOA HUDUMA YA MAOMBI KANISANI HUMO MWELINZE MJINI NJOMBE.



 Waumini wa kanisa hilo wakipokea chakula cha kiroho kwa kusikiliza injili toka kwa watumishi wa Mungu kanisani hapo.
 Wachungaji wa kanisa la TAG Cefania Tweve akiwa na mchungaji wa kanisa la Pentekosti Mkoa wa Mbeya Benjamini Kivovele wakiwa kwenye mahubiri kanisani siku ya jumapili .


 Mapepo yanatolewa wengine watoa machozi ambao walivamiwa na mapepo na sasa yakutana na neno la Mungu.

Kanisa la Tanzania of Assembles Of God Mjini Njombe limeiomba serikali na taasisi za kidini kusimamia sheria zilizowekwa ili kujenga maadili mema kwa vijana kwa kupiga marufuku tabia ya baadhi ya watu wanaotumia mavazi yasiyo stahili kwa jamii pamoja na kusimamia makosa mbalimbali ikiwemo ugomvi na kujichukulia sheria mkononi.

Akiongea akiwa Mjini Njombe Mchungaji wa kanisa la Pentekost of holines assosion mision of Tanzania kutoka Mbeya Benjamini Kivovele amesema mmomonyoko wa maadili ya vijana yanayooneshwa kwa sasa yanatokana na kupuuzia kwa baadhi ya taasisi ambazo zimepewa mamlaka ya kusimamia maadili katika jamii.

Aidha mchungaji Kivovele amesema kuwa endapo jamii kwa kushirikiana na makanisa na wapenda haki pamoja na serikali ikiwemo watu wanaosimamia haki za binadamu watashikamana watakuwa na uwezo mkubwa wa kupiga marufuku mavazi yasistahili kwa jamii pamoja na vitendo vya kujichukulia sheria mkononi.


Katika hatua nyingine mchungaji Kivovele amekemea vikali ulevi kwa vijana na kusema kuwa kuporomoka kwa maadili  kunaonekana wazi katika sekta mbalimbali ikiwemo ubadhilifu  wa mali za umma unaopatikana  kwa watumishi katika baadhi ya taasisi za serikali na zisizo wa serikali ikiwemo vitendo vya rushwa.


Kwa upande wake mchungaji wa kanisa la TAG la melinze mjini Njombe amesema jukumu la kukemea maovu si la taasisi za kidini pekee bali ni la kila mmoja pamoja na serikali kupigania maadili mema na kukemea kwa nguvu zote ili kuondoa ukahaba na kupunguza maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

Watumishi wa Mungu hao wamesema kuwa chanzo cha kuharibika kwa maadili kwa wakati huu ni kutokana na huduma za vinywaji vya kilevi na mabahamedi na makahaba kuongezeka na ndiyo wanaoharibu maadili hapa nchini.

No comments:

Post a Comment