Tuesday, April 23, 2013
MKUU WA WILAYA YA NJOMBE ATEMBELEA VYANZO VYA MAJI LEO,MKUU WA WILAYA YA NJOMBE AKELWA NA UHARIBIFU WA VYANZO VYA MAJI IKIWEMO CHANZO CHA MTO LUAHA MKUU WA IRINGA.
HAPA MKUU WA WILAYA YA NJOMBE SARAH DUMBA ANAANZA SAFARI YAKE AKIANZIA MTAA WA KIBENA MADUKANI.
HII MITI NI MAOTEA INATAKIWA KUONDOLEWA NA WANANCHI NA ITATUMIKA KWA MIPANGO YA KIJIJI.
MKUU WA WILAYA AKIWA NA TIMU NZIMA YA UONGOZI WA MITAA YA KIBENA NA WATAALAMU WA MISITU HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE AKITOKA KUKAGUA CHANZO CHA MAJI KILICHOPANDWA MITI NA KAMPUNI YA TANWAT.
HAPA WAMESIMAMA KWENYE CHANZO CHA MAJI KINACHOTIRIRISHA KUELEKEA BWAWA LA LIHOGOSA LAKINI MITI IMEPANDWA NA KAMPUNI ISIYO RAFIKI KWA HADI KWENYE MAJI
HII INATAKIWA KUONDOLEWA IPO NDANI YA MITA SITINI HIVYO IONDOLEWE ALISEMA MKUU HUYO WA WILAYA.
BWAWA HILI HAPO ZAMANI MAJI YALIKUWA MENGI SANA LAKINI SASA YAMEDAIWA KUPUNGUA CHANZO WAMEHARIBU VYANZO VYAKE
ENEO HILI LIPO KATIKA KAMPUNI YA TANWAT NA MITI HII IMEPANDWA NA WAMILIKI HAO AMEAGIZA IFIKAPO WIKI IJAYO IWE HAIPO LA SIVYO ANAKWENDA MWENYEWE NA SHOKA KUKATA.
SHUGHULI ZA KAMPUNI YA TANWAT NA HIKI NI KIWANDA CHA TANWAT KINACHODAIWA KUTIRIRISHA MAJI MACHAFU KWENYE BONDI HILI AMBALO NI CHANZO CHA MTO LUAHA MKUU.
HAPA NDIPO CHANZO CHA MTO LUAHA MKUU WA IRINGA KILIPOANZIA SASA MTO HUO UMEPUNGUA MAJI KWA KIWANGO KIKUBWA NDIYO MAANA MKUUWA WILAYA SARAH DUMBA AWA MBOGO KUTETEA VYANZO HIVYO.
BI SARAH DUMBA ANATOKA KUKAGUA CHANZO CHA MAJI AMBACHO KIMEPANDWA MITI HAKIJAACHWA MITA SITINI HAPA NI MTAA WA MPETO.
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi Sara Dumba Ametoa Muda wa Wiki Moja Kwa Halmashauri ya Mji wa Njombe, Kuhakikisha Inasimamia Uboreshaji wa Mazingira Katika Vyanzo Vya Maji Vya Mto Ruaha Mkuu, Pamoja na Kulinda Vyanzo Vya Maji Vilivyo Hatarini Kutoweka Kwenye Eneo Hilo.
Aidha Mkuu Huyo wa Wilaya Ameagiza Kuchukuliwa Kwa Hatua za Utekelezaji Ili Kulinda Vyanzo Vya Maji Vilivyoharibiwa na Kusema Kuwa Miongoni Mwa Hatua Zinazopaswa Kuchukuliwa, ni Pamoja na Kuondolewa Kwa Miti Inayoharibu Mazingira Katika Eneo Hilo.
Akizungumza Mara Baada ya Kutembelea Vyanzo Vya Maji Vinavyotiririsha Maji Katika Mto Ruaha Mkuu,Mkuu Huyo wa Wilaya Amewataka Watendaji Hao Kuhakikisha Vyanzo Vyote Vya Mto Ruaha Mkuu Vinakuwa Katika Hali Yake ya Kawaida.
Amesema Katika Mto Ruaha Mkuu Wamekubaliana na Halmashauri Kuwa Watapanda Miti Rafiki wa Maji Pamoja na Kuwataka Watendaji Hao Kukutana na Uongozi wa Kampuni ya TANWATI Ili Kudhibiti Maji Yanayotoka Kwenye Viwanda Vya Kampuni Hiyo Ambavyo Vimekuwa Vikitiririsha Maji Machafu Kwenye Vyanzo Hivyo.
Kwa Kutambua Ukubwa wa Tatizo la Maji Mjini Njombe Linalotokana na Kuongezeka Kwa Uharibifu wa Vyanzo Vya Maji,Mkuu wa Wilaya Anasema Huu Sio Mwisho na Badala Yake Wataendelea Kukagua Uharibifu Wowote Unaofanyika Ili Kuwachukulia Hatua Kali Wahusika.
Kwa Upande Wao Watendaji Walioongozana na Mkuu wa Wilaya Kwenye Ziara Hiyo,Pamoja na Kukiri Juu ya Kuwepo Kwa Tatizo Kubwa la Uharibifu wa Mazingiera Lililofanyika Kwenye Eneo Hilo Lakini Pia Wameahidi Kuchukua Hatua Stahiki Kama Ilivyoagizwa na Mkuu wa Wilaya.
Kumekuwa na Ongezeko la Matukio ya Uharibifu wa Vyanzo Vya Maji Mkoani Njombe,Jambo Linalosababisha Kupungua Kwa Kiwango Cha Maji na Kusababisha Tatizo la Maji Katika Maeneo Mbalimbali Ukiwemo Mji wa Njombe.
Takribani mwezi mmoja kampuni ya TANWAT ilikili kukiuka taratibu za utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti isiyo rafiki wa maji na kuwaahidi wananchi kwamba miti hiyo itavunwa haraka iwezekanavyo lakini mpaka sasa bado jitihada hizo zinaendelea.
Siku cha che zilizopita baraza la maendleo la kata yan Ikuna liliazimia kuweka kakati ya kuhakikisha serikali za vijiji zinakata miti yote iliyoota kimakosa na kuwashinikiza waliopanda isiyo rafiki kwa vyanzo vya maji kinyume na sheria kuondoa miti yao kwani ni chanzo cha kusababisha maji kukosekana mkoani Njombe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment