YANGA HAIKAMATIKI, YAICHAPA RUVU SHOOTING 1-0 NA KUZIDI KUJIKITA KILELENI
"Pisha pisha Yanga inapita"
"Pisha Njia Yanga inapita"
"Pisha pisha Mabingwa wanapita"
Hivyo
ndivyo washabiki, wapenzi na wanachama wa klabu ya Young Africans
Sports Club leo walivyokua wakiimba mara baada ya kumalizika kwa mchezo
wa Ligi Kuu ya Vodacom, ambapo Yanga imeweza kushinda mchezo wa tano
mfululizo kwa kuifunga Ruvu Shooting kwa bao 1- 0, mchezo uliofanyika
katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Young Africans
imeendelea kujiweka katika nafasi nzuri ya msimamo wa Ligi Kuu ya
Vodacom baada kufikisha point 48 na mabao 37 ya kufunga, pointi 11 mbele
ya timu inayoshika nafasi ya pili Azam Fc yenye pointi 37 huku Yanga
ikiwa mbele kwa mchezo mmoja.
Kikosi cha
mholanzi Ernest Brandts kiliuanza mchezo kwa kasi na katika dakika ya
15 mshambuliaji Nizar Khalfani alikosa bao la wazi kufuatia kuwatoka
walinzi wa timu ya Ruvu Shooting lakini shuti alilopiga lilitoka
sentimeta chache ya lango la Ruvu Shooting.
Ruvu
Shooting ilicheza soka la kushambulia kwa kushitukiza na kupitia
washambuliaji wake Hassani Dilunga, Said Dilunga na Antony Kiiyala na
katika dakika ya 24 ya mchezo Said Dilunga alikosa bao la wazi kufuatia
kubakia yeye na mlinda mlango wa Yanga Ally Mustafa 'Barthez'.
Saimon
Msuva alikosa nafasi ya kuipatia Young Africans bao la mapema kufuatia
kutokua makini katika umaliziaji kufutia kupewa pasi safi nzuri na
kiungo Frank Domayo lakini umakini wa Msuva ulipelekea kukosa bao hilo
la wazi.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza, Ruvu Shooting 0 - 0 Young Africans.
Kipindi
cha pili kilianza kwa Yanga kufanya mabadiliko ambayo yaliipelekea
Yanga kuimarika na kuutawala sehemu ya kiungo kwani kuingia kwa Luhende
kuliongeza kasi ya mashambulizi kwa timu ya Yanga,
Dakika
ya 48 ya mchezo, Hamis Kiiza aliipatia Young Africans bao la kwanza na
bao la ushindi pekee katika mchezo huo kufuatia kumalizia mpira
uliopigwa na Nizar Khalfani kumpita kipa Benjamin Haule na walinzi wake
kisha kumkuta Kiiza aliyeukwamisha wavuni bila ajizi.
Kufuatia
bao hilo, Ruvu Shooting walibadilika na kufanya mashambulizi ya kusaka
bao la kusawazisha lakini umakini wa walinzi wa Yanga wakiongozwa na
Nadir Haroub 'Cannavaro' na Mbuyu Twite ulikua kikwazo kwao kuweza
kuipenya ngome hiyo.
Mshambuliaji Nizar Khalfani
aliumia mguu kufuatia kukanyagwa na mlinzi wa Ruvu Shooting Shaban
Ibrahim aliyemchezea ndivyo sivyo, kufuatia maumivu hayo Nizar alitolewa
nje na nafasi yake kuchukuliwa na Didier Kavumbagu.
Mbadiliko hayo hayakubadili ubao wa matokeo, kwani mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Ruvu Shooting 0 - 1 Young Africans.
Kocha
mkuu wa Yanga Ernest Brandts amesema anashukuru timu yake kupata kwa
ushindi katika mchezo wa leo, kipindi cha kwanza timu yangu haikucheza
vizuri , lakini kipindi cha pili nilifanya mabadiliko na kubadili mfumo
wa uchezaji hali iliyopelekea kupata bao hilo la ushindi.
"Kikubwa
tulikuwa tunahitaji ushindi wa pointi 3 amabzo tumefanikiwa kuzipata,
kila mchezo kwetu ni fainali ili kujiweka katika mazingira mazuri ya
kutwaa Ubingwa, inabidi tushinde kila mchezo na ninashukru tumeshinda,
tunajiandaa na mchezo dhidi ya Polisi Morogoro mwishoni mwa mwezi siku
ya jumamos ya tarehe 30.03.2013" alisema Brandts
Baada
ya mchezo huu wa leo kocha wa Young Africans Brandts ametoa mapumziko
ya siku tatu (3) kwa wachezaji ili waweze kupumzika na familia zao, na
timu itaanza tena mazoezi siku ya jumatano kujiandaa na mchezo huo dhidi
ya Polisi Morogoro utakaofanyika katika uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Young Africans:
1.Ally Mustapha 'Barthez', 2.Juma Abdul, 3.Oscar Joshua/David Luhende,
4.Nadir Haroub'Cannavaro', 5.Mbuyu Twite , 6.Athuman Idd 'Chuji',
7.Saimon Msuva, 8.Frank Domayo, 9.Nizar Khalfani /Didier
Kavumbagu,10.Hamis Kiiza, 11.Haruna Niyonzima
No comments:
Post a Comment