Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Saturday, March 16, 2013

KAMATI YA USHAURI WILAYA YA NJOMBE DCC YAFANYA ZIARA NINGA NA KICHIWA NJOMBE

.
 Wanafunzi wa shule ya msingi Ninga wakiwa Mistari wakati mkuu wa wilaya ya Njombe alipo wasili shuleni hapo.
 Mkazi wa kijiji cha Kichiwa akipokea fedha shilingi Elfu Hamsini zilizotolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Njombe Mh. Valence Kabelege kwa ajili ya maji ya visima.
 Katibu tawala wa wilaya ya Njombe Evagrey Keiya akimkaribisha mwenyekiti wa kamati ya ushauri ya wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba kuzungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Kichiwa ili kubaini changamoto zinazo wakabili.
 Wanafunzi wa shule ya msingi Kichiwa wakiwa mistarini tayari kwa kumsikiliza Mwenyekiti wa DCC Njombe.

 hAWA ni wanafunzi wa shule ya msingi Kichiwa wakiwa wamekaa chini wakimsikiliza mwenyekiti wa kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba wakati wa ziara ya kikazi.
 Hapa ni wajumbe wa kamati ya ushauri ya wilaya ya Njombe ikiwa katika kijiji cha Kichiwa jana.
 hAWA ni wanafunzi wa shule mpya ya Ninga sekondari iliyoanza rasmi februari 18 mwaka huu wakimsikiliza Mkuu wa wialaya ya Njombe alipowatembelea Jana shuleni kwao.
 Kushoto ni mkuu wa wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba akiwa darasani katika shule ya sekondari Ninga wakati wa Ziara ya Kamati ya Ushauri ya wilaya ya Njombe.

Hawa wote ni wanafunzi wa shule moja.

Kamati ya ushauri ya wilaya ya Njombe jana imefanya ziara ya kuwatembelea wananchi katika vijiji mbalimbali wilayani Humo ili kubaini changamoto mbalimbali zinazo wakabili wananchi kwa mustakabali wa taifa.

Ziara hiyo iliyoongozwa na mwenyekiti wake Bi.Sarah Dumba ambaye ni mkuu wa wilaya ya Njombe kwa siku ya jana imefanyika katika vijiji vya kichiwa na Ninga kwa kuzungumza na wanafunzi wa shule ya Msingi Kichiwa pamoja na wananchi wa kijiji hicho na kisha kubaini changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi na wanafunzi wa kijiji hicho.

Akiwa katika shule ya msingi Kichiwa mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Dumba amebaini changamoto mbalimbali kutoka kwa wanafunzi wa shule hiyo ikiwemo baadhi ya wazazi kugoma kuchangia chakula cha wanafunzi shuleni pamoja na uchakavu wa majengo na vyoo vya shule hiyo.

Evagrey Keiya ni katibu tawala wa wilaya ya Njombe ambaye amesema kuwa lengo la ziara ya kamati hiyo ya ushauri ni kutaka kupata kero mbalimbali zinazowakabili wananchi kiujumla ikiwemo migogoro ya ardhi,mifarakano katika familia ili kujadili na kuzipatia ufumbuzi hususani kwa akina mama na watoto.

Baada ya katibu tawala kueleza lengo la kamati hiyo kuzukungia vijijini ndipo mkuu wa wilaya ya Njombe akatoa agizo kwa wazazi kuhakikisha wanapeleka chakula kwa watoto wao shuleni ili kuepusha adha wanayoipata baadhi ya wanafunzi pamoja na kuhakikisha wanajenga vyoo vya shule hiyo.
 
Katika hatua nyingine pia amezungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Ninga katika kata ya Ninga pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Ninga na kisha kuhamasisha ujenzi wa madarasa na nyumba za walimu katika shule ya sekondari Ninga ambayo hadi sasa haina hata nyumba moja ya mwalimu kutokana na kuanzishwa mapema februari mwaka huu na kuwa na kidato cha kwanza pekee.

Hata hivyo ziara kama hiyo itafanyika tena machi 16 mwaka huu kwa kuzungumza na wananchi wa Kijiji cha Matembwe na kisha kuhitimisha katika kijiji cha Lupembe ambako yatafanyika majumuisho ya ziara hiyo ili kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo na kuzipatia ufumbuzi zaidi.

No comments:

Post a Comment