Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Saturday, March 16, 2013

SHILINGI MILIONI 25.5 ZATUMIKA KUJENGA JENGO JIPYA LA UHAMIAJI NJOMBE.

 Limefunguliwa  na katibu tawala mkoa wa Njombe Bi.Mgeni Baruan kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Njombe.
 Katibu tawala mkoa wa Njombe Bi.Mgeni Baruani Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe akizindua jengo jipya la Uhamiaji Wilaya ya Njombe Leo.
 Jengo la uhamiaji wilaya ya Njombe mara baada ya kuzinduliwa rasmi na katibu tawala mkoa wa Njombe leo
 Hii ni kwaya Toka mjini Makambako ikifanya vyema wakati wa uzinduzi wa Jengo la uhamiaji.
 Bi.Rose Mhagama Naibu kamishna uhamiaji Njombe akizungumza mara baada ya kuzinduliwa kwa jengo lao
 Katibu tawala mkoa wa Njombe ampongezi Naibu kamishna wa uhamiaji mkoa wa Njombe Bi.Rose Mhagama kwa kujenga jengo kwa gharama ndogo.
 Mgeni rasmi Bi.Mgeni Baruan Akiondoka mara baada ya Kuzindua jengo hilo lililotumi shilingi milioni 25.5 TU kwa usimamizi wa Naibu kamishna wa uhamiaji Mkoa wa Njombe Bi.Rose Mhagama.
 Hawa ni baadhi tu ya maafisa uhamiaji mkoa na wilaya ya Njombe wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Huu ni muonekano wa Jengo jipya na lazamani upande wa kulia baada ya Uzinduzi.

Jumla ya shilingi milioni 25.5 zimetumika katika ujenzi wa Jengo jipya la ofisi za uhamiaji wilayani Njombe kufuatia kuchakaa kwa ofisi hizo.

Taarifa hiyo imebainishwa leo wakati www.gabrielkilamlya.blogspot.com ilipo shuhudia uzinduzi wa jengo hilo katika ofisi za uhamiaji Njombe na kwamba jitihada za Naibu kamishna wa uhamiaji mkoa wa Njombe Bi.Rose Mhagama ndizo zilizofanikisha kujengwa kwa jengo hilo.

Awali akizungumza kabla ya uzinduzi wa jengo hilo Kamishna wa utawala na Fedha bwana Peniel Mgonja amesema kuwa pamoja na wizara hiyo kutoa fedha kidogo zilizoombwa kwa ajili ya ukarabati lakini Kamishna Bi.Rose Mhagama amefaniwa kujenga jengo jipya litakalo wasaidia katika kipindi hiki.

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Njombe katibu tawala wa mkoa wa Njombe Bi.Mgeni Baruan Amesema kuwa pamoja na wizara hiyo ya mambo ya ndani Idara ya Uhamiaji kuwezesha fedha za jengo hilo lakini pia amemuomba kamishna wa Utawala na Fedha kuwasaidia katika ujenzi wa jengo kubwa la uhamiaji mkoa kufuatia kuanzishwa kwa mkoa wa Njombe.
 
Uzinduzi huo unaambatana na hafla ya kumpongezi Bi.Rose Mhagama kwa jitihada kubwa alizozifanya katika kufanikisha ujenzi huo zitakazofanyika katika ukumbi wa Day to Day Kibena leo jioni.

No comments:

Post a Comment