Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Saturday, March 16, 2013

MADALALI NJOMBE WATAKA BIASHARA YA RUMBESA IPIGWE MARUFUKU KOTE NCHINI.



 MJUMBE WA HALMASHAURIM KUU YA CCM TAIFA WILAYA YA NJOMBE  NA DIWANI WA KATA YA NJOMBE MJINI LUPYANA FUTE.

 MWENYEKITI WA MADALALI NJOMBE AKIZUNGUMZA KATIKA KIKAO KILICHOFANYIKA MJININ NJOMBE.MATHIAS LUFUNYO.



 MADALALI WA NJOMBE MJINI WAKIWA KWENYE KIKAO NA MJUMBE WA HALMASHAURI KUU CCM TAIFA WILAYA YA NJOMBE NA DIWANI WA KATA YA NJOMBE MJINI.






 


 VIONGOZI WA SE5RIKALI YA MTAA WA KWIVAHA NA KATA YA NJOMBE MJINI  WAKIWA KWENYE MJADALA.picha na Michael Ngilangwa.




Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi CCM wilayani  Njombe Bw Lupyana Fute Amesema Kwa Kushirikiana na Watendaji Wengine wa Serikali na Madiwani Watahakikisha Wanamaliza Tatizo la Rumbesa Ambalo Limekuwa Likilalamikiwa na Wakulima Kwa Muda Mrefu.

Akizungumza na Madalali Mjini Njombe Bw Fute, Pamoja na Kuwapongeza Madalali Hao Kwa Hatua Yao ya Kutaka Kukomeshwa Kwa Mtindo Huo Lakini Pia Anaahidi Kutumia Nafasi Yake Kama Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Kulimaliza Tatizo Hilo.

Kwa Upande Wao Madalali Waliohudhuri Mkutano Huo Wamesema Ili Kukomesha Mtindo Huo ni Lazima Kuwepo Kwa Ushirikiano Kati ya Watendaji na Viongozi wa Vijiji Kwa Kushirikiana na Wakulima Wenyewe Ndipo Tatizo la Rumbesa Litamalizika

Kumekuwa na Maombi ya Muda Mrefu Kwa Wakulima wa Viazi Mkoani Njombe Kuiomba Serikali Kuchukua Hatua za Kudhibiti Uuzaji wa Viazi Kwa Mtindo wa Rumbesa Jambo Ambalo Hadi Sasa Limeshindwa Kupatiwa Muafaka Licha ya Wakulima Hao Kuendelea Kunyonywa na Wafanyabiashara


Aginetha Mpangile ni diwani wa kata ya Ulembwe mwakajana alijaribu kukemea suala la biashara ya Rumbesa lakini jitihada zake ziligonga mwamba baada ya kukosa ushirikiano toka kwa viongozi wengine wa kata na serikali hali iliyopelekea biashara hiyo kuendelea hadi leo.

No comments:

Post a Comment