DR CONRAD UGONILE AKIWA OFISINI KWAKE AKIHOJIANA NA WAANDISHI WA HABARI .Picha na Michael Ngilangwa.
Wananchi wa Kijij cha Lusisi Wilaya ya Wanging'ombe
Mkoani Njombe Wamelalamiki Huduma Mbovu za Afya Zinazotolewa Katika Zahanati ya
Kijiji Hicho Hali Inayowalazimu Kufuata Huduma Hiyo Vijiji Vya Jirani.
Aidha Wananchi Hao Wamelalamikia Ukosefu Mkubwa wa Dawa
Unaoikabili Zahanati Hiyo Hali Ambayo Huwalazimu Kununua Dawa Hizo Katika
Maduka Binafsi.
Mwenyekiti wa Kijiji Hicho Bw Jaktan Mwanyika Anakiri
Kupokea Malalamiko Hayo ya Wananchi na Kusema Kuwa Wanatarajia Kuyafikisha
Katika Ngazi Husika Ili Kuweza Kuyapatia Ufumbuzi.
Conrad Ugonile ni Kaimu Mganga Mkuu Halmashauri ya Wilaya
ya Njombe Pamoja na Kukiri Kutopokea Malalamiko Hayo ya Wananchi Lakini Pia
Anatumia Fursa Hiyo Kuelezea Utaratibu wa Usambazwaji wa Dawa Katika Zahanati
Wilayani Njombe.
Kwa Mujibu wa Dokta Ugonile Zahanati ya Kijiji Cha Lusisi
Kwa Mara ya Mwisho Ilipatiwa Dawa Januari 20 Mwaka Huu na Inatarajiwa Kupatiwa
Dawa Tena Mwezi Aprili Mwaka Huu.
No comments:
Post a Comment