Apigwa na nondo usiku baada yakukataa kuachia pikipiki waende nayo wanaodhani ni majambazi.
Huyu nae alivamiwa na majambazi walipomtaka aachie pikipiki aliwaachia ndipo wakamfunga na kamba kwenye miti na kuchukua pikipiki lakini zote pikipiki mbili zilikutwa zimefichwa kwenye kichaka eneo la uwanja wandege.
Huyu ni mwenyekiti bodaboda mkoa wa Njombe Abed Mgaya anasema amesikitishwa sana na wizi wa Njuombe.
Kikao cha dharula cha itishwa na wamili na waendesha pikipiki maarufu bodaboda Njombe kuimarisha usalama wao pamoja na kuwabaini wanaohusika na mauaji ya nondo.
ACP Fulgence Ngonyani akatoa ahadi ya kuonesha ushirikiano na kuwapongeza kwa hatua waliofikia madereva hao.
Madereva Pikipiki Maarufu Kama Bodaboda Mkoani Njombe
Wameiomba Serikari Kuimarisha Ulinzi na Usalama Nyakati za Usiku Katika Vituo
Vyao vya Kazi Ili Kuweza Kukabiliana na Matukio ya Uhalifu na Uporaji Pikipiki
Yalioanza Kujitokeza Mkoani Hapa
Wakizungumza Wakati wa Kikao Cha Madereva Hao
Kilichofanyika Katika Viwanja Vya NHC Mjini Njombe Madereva Hao Wamesema Kuwa
Kitendo Cha Kuanza Kujitokeza Kwa Matukio Hayo Kimeanza Kuwapa Wasiwasi na
Hivyo Huenda Kikakwamisha Shughuli Zao na Kuzorotesha Uchumi wa Mkoa
Wamesema kuanzia sasa watakuwa wanaweka doria kila mahali ili kuhakikisha uharifu hususani wizi wa pikipiki unatokomea na kuwakamata wanaohusika na vitendo hivyo vya wizi na mauaji ya kutumia nondo mjini Njombe.
Mwenyekiti wa Madereva Pikipiki Mkoa wa Njombe Bwana Abed
Mgaya Anasema Hadi Kufikia Sasa Zaidi ya Matukio Mawili ya Uvamizi Kwa Madereva
Yameshajitokeza na Kusababisha Upotevu wa Mali za Madereva
Hatahivyo Bwana Abed Mgaya Ametoa Wito Kwa Madereva
Pikipiki Kuwa na Ushirikiano Baina yao Kwa Kuhakikisha Wanakuwa na Vitamburisho
na Kuwa na usajili wa Pikipiki Zao ili Kuweza Kuwabaini Waarifu na Wasiokuwa na
leseni huki madereva hao wakiazimia kuweka doria maeneo ambayo vibaka hao
wanaojificha ili kutokomeza uharifu mkoani hapa.
Kwa upande wake kamanda wa jeshi la polisi mkoani Njombe
ACP Fulgenzi Ngonyani amekili kupokea taarifa za upolwaji wakutumia silaha aina
ya nondo na kusema kuwa jeshi la polisi litawaunga mkono wamiliki na madereva
wa bodaboda katika kuweka doria juu ya uharifu ulioanza kujitokeza.
No comments:
Post a Comment