WACHUNGAJI,MAPADRE NA MAHSEHE WAKIWA KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA NCHI.
HOTUBA YA WAKILI WA SERIKALI BWANA ABIMAK MABROUK MBELE YA MGENI RASMKI.
MGENI RASMI AKITOA HOTUBA YA ERNEST MKONGE MBELE YA WADAU WA SHERIA MKOA WA NJOMBE
HAKIMU WA MAHAKAMA YA WILAYA YA NJOMBE RWANZILE AKITOA HOTUBA MBELE YA MGENI RASMI SIKU YA SHERIA NCHINI.
PICHA ZA PAMOJA NA WATUMISHI MBALIMBALI WAKIWEMO WATUMISHI WA MUNGU.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Captain Mstaafu Asseri Msangi
ameviomba vyombo vya maamuzi vya sheria pamoja na viongozi wa mkoa na wilaya
kuwa karibu na wananchi na kutoa huduma za kutendewa haki kwa karibu zaidi
kuliko ilivyo sasa ili kuwaridhisha wananchi na maendeleo yasonge mbele katika
mkoa wa Njombe.
Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Njombe katika
maadhimisho ya siku ya sheria nchini kaimu katibu tawala wa uchumi na
uzalishaji mkoa wa Njombe Ernest Mkonge amesema mkoa wa Njombe unakabiliwa na
changamoto kubwa ya ukosefu wa mahakama na mahakimu wa wilaya na mwanzo Ambapo
ametaja ushirikiano kwa viongozi ili kutatua tatizo hilo.
Katika hotuba yake bwana Mkonge amewataja viongozi wa
dini na siasa kuwa wanaushawishi mkubwa kwa wananchi na kuwaomba wananchi kuzitii sheria za nchi zilizopo
ambazo hazikinzani na sheria zilizowekwa na nchi kupitia mahubili yao ili
kulinda amani na utulivu ikiwa ni pamoja na kukemea maovu yote ya
mauaji,rushwa na ujambazi ili wananchi
watii sheria na kudumisha utawala wa sheria.
Akitoa hotuba ya mahakama ya wilaya ya Njombe hakimu
mkazi Mfawidhi Mwandamizi wilaya ya
Njombe Augustino Rwanzile amesema kwa kawaida somo la utawala wa sheria ni pana
sana na kusema kuwa haliishii katika kutekeleza sheria zilizopo bali linakwenda
mbali zaidi na kuangalia kama sheria zenyewe ni za haki.
Lakini katika hotuba yake bwana Rwanzile imeanisha mambo
muhimu yanayoweza kutoa ufafanuzi jadidifu
kwamba kwa sasa nchi yetu imekumbwa na wimbi kubwa la mmomonyoko wa
maadili ufisadi, vitendo vya
rushwa,kujilimbikizia mali sivyo halali,kutowajibika kwa viongozi na watumishi
wa umma,utomvu wa nidhamu,matumizi mabaya ya madaraka ambapo hayo yote
yanasababishwa na kutotekelezwa kwa sheria zilizopo.
Amesema katika muktadha huo uhuru na usawa wa raia kwa maoni yake ni musingi muhimu wa utawala
wa sheria ambapo kwa sasa kuna maswali
mengi ya kujiuliza kama.
Je? kuna uhuru na usawa wa raia katika jamii ya sasa ya
mtanzania?
Je? nchi yetu inafuata utawala wa sheria?
Je? shereia zilizopo zinatekelezwa ipasavyo?
Nas je? sheria zenyewe ni za haki ama kandamizi? ambapo
katika kujibu maswali hayo alijaribu kueleza viashiria vya maswali hayo kwamba
Huko Karatu
Mtanzania mmoja alikamatwa baada ya kushtukiwa kuiba simu watu wenye hasira
kali walimkata masikio na kumlazimisha ayale na baada ya kuyala wakamuua na
kumchoma moto baada ya hapo wakatawanyika,huko Ngala wa jeshi la polisi walimkamata mtuhumiwa wa makosa ya usalaama
barabarani katika kubishana kati ya askali wawili na mtuhumiwa wao askali mmoja
akaamua kumupiga risasi mtuhumiwa na kumuua baada ya hapo wananchi
walijikusanya na kwenda kuwauwa askali polisi hao na kwenda kuteketeza kituo
cha polisi.
Alisema Iringa askali wakavamia mkutano wa siasa na
wananchi wakatawanyika mwandishi wa habari aliyekuwa akirekodi matukio kati ya
askali na raia akazingirwa na polisi akauwawa, katika mkoa wa Mara TFDA waligundua dawa za za kufubaza virusi vya
UKIMWI lakini uchunguzi ukabainisha dawa hizo zimesambazwa nchi nzima na
waathilika wamekuwa wakizitimia kiwanda hicho kinamilikiwa na Mtanzania mmoja
kwa kushirikiana na serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na baada ya Mgogoro huu mmiliki wa kiwanda
hicho akachaguliwa kuwa mwenyekiti wa
chama cha siasa katika mkoa wa Dar es Salaam.
Bwana Rwanzile Alisema Yapo mengi aliyoyasema lakini kwa
maoni yake amesema pengine hayo yote ni matokeo ya kupuuza utwala wa sheria.
Abimaki Mabrouk Amesema ili kuimarisha msingi madhubuti
na imara wa utawala wa sheria nchini umoja kwa pamoja inatakiwa kuwa na nia na
nguvu zaidi ya kuzuia,kupambana na kutokomeza adui rushwa ambalo ni janga la
kitaifa.
Amesema serikali,taasisi zake,vyombo vya dola na
watendaji wake ni lazima waichukie,kuikemea na kuiongopa kama ukoma ikiwa ni
pamoja na kuchukuliwa hatua kali za kisheria
na kwa uwazi bila kujali vyeo,mali,umaarufu,dini,rangi na makabila kwa
watoaji,wanaoomba na wapokeaji rushwa.
Pamoja na hayo bwana Mabrouk amesema serikali inatakiwa kuangalia namna ya
kuboaresha maslahi duni ya watumishi wa
serikali hasa wale wanaohusika moja kwa moja na usimamiaji na utekelezaji wa
sheria ikiwemo jeshi la polisi,mahakama,mawakili wa serikali na watendaji wa
mfumo mzima wa haki jinai huku akisema mishahara,motisha na mazingira ya kazi
viboreshwe kukidhi mahitaji na gharama
za kimaisha.
No comments:
Post a Comment