Wazee wanampokea kijana ambae alikuwa mjumbe wa CHADEMA Braiton Mbajo na sasa kahamia CCM kata ya Ubena Makambako.
Kijana Braiton Mbajo akitoa sababu yakuhama chama cha CHADEMA na kuhamia chama cha mapinduzi.
Braiton Mbajo amenyosha mkono wakati wakuapishwa na katibu mwenezi wa chama chaq mapinduzi kata ya Ubena Hiltra Msolla.
Akijibu maswali yaliulizwa na wananchi wa Ubena mjumbe wa halmashauri kuu ccm Taifa wa Wilaya ya Njombe Lupyana Fute.
Baada ya kumaliza mkutano katika kata ya Ubena sasa wanarejea majumbani kwao na hapa ni ofisi ya kijiji cha Ubena Makambako.
Wananchi wa Kata ya Ubena Mkoani Njombe Wameitaka
Serikali Kusimamia Vema Ujenzi wa Miradi ya Maendeleo Ikiwemo Kuchagua
Makandarasi Wenye Sifa Ili Kuondokana na Tatizo la Kuharibika Mara Kwa Mara Kwa
Miradi Hiyo Muda Mfupi Baada ya Kuanza Kutumika.
Miongoni Mwa Miradi Inayolalamikiwa ni Pamoja na Ile ya
Maji na Barabara Ambayo Imekuwa Ikiharibika Muda Mfupi Baada ya Kuanza Kutumika
Jambo Linalosababisha Hasara Kwa Wananchi na Serikali.
Wakizungumza Wakati wa Mkutano wa Hadhara Uliofanyika
Kwenye Kata Hiyo Ikiwa ni Sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 36 ya Kuzaliwa Kwa
Chama Cha Mapinduzi CCM,Wananchi Hao Wamesema Kuwa Bado Kumekuwa na Tatizo la
Maji Huku Kukiwa Hakuna Jitihada Zozote za Kutumia Vyanzo Vilivyopo Kutatua
Tatizo Hilo.
Aidha wananchi hao wamebainisha changamoto nyingine zinazo wakabili kuwa ni pamoja na ukosefu wa soko la kupata mahitaji hali inayopelekea kusafiri umbali mrefu ikiwa jitihada zao za kuomba kwa serikali yao lakini hakuna majubu yakuridhisha ambapo kauli hiyo waliitoa mbele ya mjumbe huyo wa halmashauri kuu ya ccm taifa wa wilaya ya Njombe NEC.
Lupyana Fute ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM
Wilaya ya Njombe Anasimama Kwenye Mkutano Huo na Kutoa Somo Kuhusu Majukumu ya
Viongozi wa Halmashauri,Kata na Vijiji.
Katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi kata ya Ubena
makambako bwana Hiltra Msolla Anatoa Tahadhari Kwa Maafisa Ardhi
Kuweza Kusimamia Vema Zoezi la Upimaji Ardhi Linalotarajiwa Kufanyika Hivi
Karibuni Kwa Kuhepusha Migogoro Inayoweza Kujitokeza
No comments:
Post a Comment