Mganga mkuu mwenye shati nyeupe dr Mgina akiuongoza ugeni kwenye mawodi hayo kwaajili ya kuwasalimu wagonjwa.
MJUMBE HALMASHAURI KUU CCM TAIFA WILAYA YA NJOMBE AKITOKA KUTEMBELEA WODI MPYA LA WANAUME MAKAMBAKO.
Haya ni mawodi mapya ya wagonjwa ambayo yamejengwa mwakajana na mengine bado yanaendelea kujengwa.
Hii ni ziara ya mjumbe wa halmashauri kuu ya ccm taifa wilaya ya Njombe Lupyana Fute akitembelea wagonjwa na kuangalia majengo mbalimbali yanayojengwa katika kituo cha afya mjakambako.
Mjumbe halmashauri kuu ccm taifa wa wilaya ya Njombe amegundua jengo la xlay likiwa chini ya kiwango na hapa anaona jengo bado kutumika lakini rangi imebanduka na kuagiza lirudiwe tena.
Jengo jipya la kisasa ambalo limejengwa kwaajili ya huduma za xlay Makambako mkoani Njombe.
Jengo dogo hilo ndilo lilikuwa chumba cha mochwali makambako kabla hawajajenga mochwali ya kisasa mwakajana Makambako.
Lupyana Fute anamalizia ziara yake ya kutembelea wagonjwa mawodini na kuwapatia zawadi ya sabuni kila mgonjwa.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Njombe Lupyana Fute
Ametembelea Kituo cha Afya cha Makambako na Kuiomba Serikali Kuelekeza Nguvu
Zake Katika Kuboresha Huduma za Afya Zinazotolewa Kwenye Zahanati na Vituo Vya
Afya Vilivyoko Maeneo ya Vijijini.
Akiwa Kituoni Hapo Mjumbe Huyo Amebaini Kuwepo Kwa
Changamoto Mbalimbali Katika Kituo Hicho Ikiwemo Uhaba wa Dawa na Vifaa Tiba
Pamoja na Upungufu wa Watumishi Hali Ambayo Inapelekea Wagonjwa Wanaofika
Katika Kituo Hicho Kupata Huduma za Afya Kutoa Lawama Kwa Uongozi wa Kituo
Hicho.
Mara Baada ya Kupokea Malalamiko Kutoka Kwa Baadhi ya
Wagonjwa Wanaopatiwa Matibabu Katika Kituo Hicho Bwana Fute Amesema Kwa
Kushirikiana na Wataalam wa Ngazi Husika
Watasaidiana Kuhakikisa Kero Hizo Zinakwisha .
Naili Mbyompyo ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji
wa Makambako Ambaye Amekiri Kuwepo Kwa Changamoto Mbalimbali Katika Kituo cha
Afya Makambako , Ambapo Kwa Sasa Tayari Wameanza Kuzitatua Changamoto Hizo .
Akielezea Baadhi ya Changamoto Zilizopo Katika Zahanati na Vituo Vya Afya Hasa Tatizo la
Uhaba wa Dawa , Mganga Mkuu Mfawidhi wa
Kituo Hicho Brasius Mgina Amesema Tatizo
la Uhaba na Ukosekafu wa Baadhi ya Dawa Linatokana na Bohari Kuu ya Madawa MSD
, Kwani Kwa Kiwango Fulani Hawapewi Dawa Wanazoziomba na Wakati Mwingine Hupewa
Dawa Zisizokidhi Mahitaji ya Zahanati Ama Kituo cha Afya.
"Alisema kwa mfano mwezi huu tumepewa kabox kamoja ka grovus ambako ndani yake kuna grovus mia moja kwa mwezi mzima kuhudumia wagonjwa wote waliopo katika kituo hiki cha makambako katatosha? Aliendelea kwa kusema tatizo la dawa ni la muda mrefu na hilo linasababisha waganga na manesi kuchukiwa na wagonjwa na wananchi kwa ujumloa kwamba madaktari wanauza dawa kumbe zinaletwa chache".
No comments:
Post a Comment