KILA KITU WAZI WIKI HII ,HIZI NDIZO DHULUMA WAZOFANYIWA WASTAAFU WA MFUKO WA HIFADHI YA JAMII WA NSSF.
Yafuatayo ni malalamiko yangu na ambayo pia ni malalamiko ya wastaafu na wanaotarajia kustaafu ambao ni wanachama wa NSSF.
Ninachoamini ni kuwa wananchi wote wanachama wa mifuko ya hifadhi ya
jamii wanayo haki ya kupata mafao sawa kwani mifuko yote iliundwa kwa
sheria zilizopitishwa na Bunge.
Cha kushangaza ni kuona jinsi mifuko hii inavyowabagua Watanzania ikiwa
na maana Bunge lilitunga sheria za kuwabagua Watanzania.
Napenda nieleze jinsi mfuko wa NSSF unavyowadhulumu wastaafu na kuulinganisha na mfuko wa PSPF.
(a) Mwanachama wa NSSF anachangia kwenye mfuko 10% ya mshahara wake kwa mwezi na mwajiri kumchangia kwa kiasi hicho.
Mwanacha wa mfuko wa PSPF anachangia kwenye mfuko 5% ya mshahara wake kwa mwezi na mwajiri kumwekea 15%.
Hii ina maana kuwa mshahara baada ya makato (net salary) anaopata
mwanachama wa NSSF ni pungufu kuliko anaopata mwanachama wa PSPF ingawa
wana mshahara ulio sawa.
(b) Mifuko yote inawekeza na uwekezaji mkubwa unafanywa na NSSF hivi
kujipatia faida kubwa. Manufaa ya uwekezaji huu ni kwa watanzania wote
na hata kwa wale ambao sii wanachama wa mifuko.
(c) Wanachama wa NSSF na PSPF wanalipa kodi sawa kilingana na
mshahara.
(d) Mafao ya uzeeni:
Inasikitisha na inatisha sana kuona jinsi mifuko hii inavyowabagua
Watanzania ikiwa na maana ya kubaguliwa na Bunge pamoja na serikali
kinyume na katiba ya nchi.
Hii ilitokana na Bunge kukubaliana na formula za ukokotoaji wa mafao ya
uzeeni ambazo zimepishana sana wakifaidi kikubwa wanachama wa PSPF.
Naomba nitoe mfano halisi wa mstaafu mwanachama wa NSSF.
(i) Alistaafu tarehe 30/6/2012 baada ya kuchangia
kwenye mfuko wa NPF na baadaye NSSF kuanzia 30/6/1988 kwa jumla ya miaka
24(miezi 288). Mshahara wake wa mwisho ukiwa sh.1,830,000 kwa mwezi.
Kiasi alichochagia kwa kipindi hicho ni sh.25,387,924 kabla ya kuweka
faida na ukiweka faida ni zaidi ya sh.28,000,000.
(ii) NSSF ilimlipa fedha ya mkupuo (commuted pension
gratuity) sh.9,805,908.32 na pensheni ya kila mwezi sh.408,621.18.
Hii ina maana kuwa ili achukue fedha zake zote zilizoko NSSF itamchukua
miezi 44 sawa na miaka 4. Hii ni dhuluma ya hali ya juu.
(iii) Mwanachama wa PSPF aliyestaafu wakati mmoja na yeye
na mwenye mshahara, kisomo na muda wa kuchangia kwenye mfuko sawa na
yeye amepewa fedha za mkupuo (commuted gratuity) sh.90,782,284.80 na
pensheni ya kila mwezi sh.488,076.80.
Hembu angalia tofauti hii na ubaguzi wa hali ya juu wa Watanzania
(e) Wahadhiri wa vyuo vikuu walio wanachama wa NSSF na PPF waligoma
kutokana na mafao kidogo yanayotolewa na mifuko hiyo ukilinganisha na
yale yanayotolewa na PSPF.
Serikali ilisikia kilio chao na aidha kuwahamisha kwenye mifuko hiyo
kandamizi na kuwafanya wanachama wa PSPF au kubadilisha formula ya
ukokotoaji wa mafao yao ya uzeeni. Hili lilithibitishwa na waziri wa
elimu na mafunzo ya ufundi katika kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na
television ya ITV.
Mbona hawa walisikilizwa na wengine kuachwa? Ubaguzi ulioje wa
Watanzania! Au ni sharti wanachama wote wa NSSF na PPF wagome ndio
wasikilizwe?
Nawalaumu wahadhiri hawa kwa kutokuwatetea wanachama wenzao.
Ninawashukuru sana wabunge kwa mchango wao uliowezesha fao la kujitoa
kurudishwa. Tunaomba hili fao la uzeeni linalowagawa Watanzani lifanyiwe
kazi mapema na wale ambao wameshaathirika wafikiriwe.
(f) Mamlaka ya kusimamia mifuko ya hifadhi jamii (SSRA)
ilianzishwa kwa sheria ya bunge. Tuliamini na kutiwa moyo kuwa mamlaka
hii ingeondoa tofauti kubwa zinazojitokeza kwenye mifuko katika utoaji
wa mafao ya uzeeni lakini tokea kuanzishwa kwake mamlaka haijatekeleza
jukumu hili.
Naomba kilio chetu kifike bungeni na naomba marekebisho ya mafao ya uzeeni yaanzie pale mamlaka hii ilipoundwa.
(g) Mheshimiwa Zitto Kabwe,mbunge, ni mmoja wa wageni rasmi walioalikwa kuhudhuria mkutano wa tatu wa wadau wa wa NSSF.
Nakuomba mfikishie taarifa hii ili alizungumzie jambo hili. Viongozi wa
NSSF wamekuwa wakiwahadaa wanachama wake kwa mambo ambayo hawayatekelezi
na wakitekeleza ni kwa kiwango cha chini sana kulinganisha na mifuko
mingine kama PSPF na mingine.
Jina na mtumaji wa wafu hii limewekwa kapuni kwa leo
No comments:
Post a Comment