Monday, February 18, 2013
MKUU WA IDARA YA MAFUNZO KATIKA SHILIKA LISILO LA KISERIKALI LA ASH TECH AHAMASISHA MATUMIZI YA VYAKULA VYA ASILI KATA YA IMALINYI.
Huu ni mfano wake na hapa akiwa katika bustani yake iliyopo kijiji cha Ilulu kata ya Imalinyi mkoani Njombe.
mstronobay umeelezwa kuwa matunda yake kuondoa sumu mwilini huku majini ikiwa ni dawa ya bipi kutibu kabisa.
Kilago akiwa katika bustani yake na hapa anawatembeza waandishi wa habari na kuwataka wananchi kutumia vyakula vya asili ambavyo vinatija.
Mkuu wa idara ya mafunzo katika shilika la ashteki mkoa wa Njombe bwana Michael Kilago amewataka wananchi kutumia zaidi vyakula vya asili ikiwemo mimea aina ya strobeli na michaichai na rozera ambayo inasaidia kukabiliana na baadhi ya magonjwa yatokanayo na chenga za chuma na vyakula vingine vyenye kuleta madhara mwilini.
Akizungumza Mkuu huyo wa Idara ya mafunzo bwana Kilago amesema ulimwengu wa sasa umejaa matatizo mengi yanayotokana na mlipuko wa magonjwa mbalimbali ambayo kwa aslimia kubwa wataalamu wamegundua kuwa yanatokana na vyakula ambavyo wanakula na kusema kuwa vyakula vingi vinavyotoka viwandani vimeambana na sumu ndizo zinazoaathili jamii.
Aidha bwana Kilago amesema Ili kukabiliana na suala zima la utunzaji mazingira wanatakiwa kushiriki kikamilifu katika kutunza mazingira kwa kupanda miti, bustani za matunda na miti mbalimbali ya mbao ambayo itawasaidia kujikwamua na hali ngumu ya umasikini .
Kwa upande wake mratibu wa shirika la Ashteki mkoa wa Njombe Atukuzwe Mwendamseke ameendelea kuhimiza wananchi kupanda miti ya mbao na rafiki kwa ufugaji wa nyuki kwa manufaa yao.
Hata hivyo bwana Mwendamseke amesema kuhusu suala la ufugaji wa nyuki katika kijiji cha Imalinyi wananchi wamelipokea vizuri ambapo amewataka vijana kuona jukumu la ufugaji wa nyuki la wote na siyo la wazee.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment