Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Friday, February 15, 2013

KWARESMA KWA WAKRISTO YAENDELEA HADI SIKU AROBAINI.



Ni kanisa katholiki parokia ya Njombe mjini wakristo waanza kwaresma siku ya jumatano ya majivu.
Waumini wakitoka kanisani huku maafisa usalama wakiimarisha usalama barabarani kutokana na umati wa wawakristo wakati wakuvuka barabara kwenye kivuko.

Wakristo Mkoani Njombe Wametakiwa Kutumia Mfungo wa Kwaresma Kutubu Dhambi Zao Kuwatembelea Wagonjwa,Watoto Yatima na Kuwasaidia Watu Wasiojiweza Kama Njia ya Kujirudi Kwa Mungu.

Aidha Wakristo Pia Wamewatakiwa Kuacha mbaya ikiwemo Uvaajimavazi Yasio na Adabu,Unyanyasaji,uvivu,Ujambazi na Kutoshiriki Anasa mbalimbali zisizompendeza Mungu

Padre wa Kanisa Katholiki Parokia ya Njombe Mjini Francisco  Chengula Amesema ibada hiyo itafanyika kwa muda wa siku mbili katika kila juma la kwanza yaani jumanne na ijumaa jioni kwa majuma 6 katika kipindi cha kwaresma.

Kwa Upandec Wao Baadhi ya Waumini Walikuwa na Maoni Kuhusu Ibada Hiyo ya Mfungo wa Kwaresma ambapo walisema hawana budi kujikita katika kuwatembelea wagonjwa na watu mbalimbali wasiyojiweza wakiwemo walemavu na wagonjwa.

No comments:

Post a Comment