Mwenyekiti wa kikundi cha Twitange cha Shamba darasa akiwa kwenye mashamba yao katika shamba walilopandia pembejeo.
Haya ni maharage ambayo hawakupandia mbolea
Wakulima wa Kijiji Cha Masaulwa Kata ya Imalinyi Mkoani Njombe Wametakiwa Kujikita Zaidi Katika Matumizi ya Zana za Kisasa za Kilimo Badala ya Kuendelea Kutumia Zana Ambazo Zimeonekana Kukosa Tija.
Aidha Maafisa Kilimo Nao Pia Wametakiwa Kuwa Karibu Zaidi na Wakulima Ili Kuweza Kuwaelimisha Kwa Usahihi Kuhusu Matumizi ya Zana Hizo Pamoja na Mambo Mbalimbali Yanayohusu Matumizi Sahihi ya Pembejeo na Mabadiliko ya Hali ya Hewa.
Neema Mgeni ni Mwenyekiti wa Kikundi Cha Twitange Kinachoshiriki Mafunzo ya Shamba Darasa Anasema Wakulima Wanaweza Kuboresha Kilimo Chao Kama Watayatumia Vema Mafunzo Hayo.
Kaimu Afisa Mtendaaji wa Kata ya Imalinyi Eusebius Mtasiwa Amewapongeza Wanakikundi Hicho cha Shamba darasa cha Twitange kwa jitihada kubwa wanazozifanya za Kuendeleza Kilimo
No comments:
Post a Comment