Thursday, February 21, 2013
DIWANI KATA YA IMALINYA AUAGIZA UONGOZI WA KIJIJI CHA MASAULWA KUMSIMAMISHA MUWEKEZAJI WA MASHAMBA YA KIJIJI ,VIONGOZI WA KIJIJI HICHO WADAIWA KUSAINIANA NA MUWEKEZAJI HUYO PASIPO KUWASHIRIKISHA WANANCHI.
WANANCHI MASAULWA WAKIWASILI KWENYE MKUTANO WA KIJIJI.
VIONGOZI WA KATA NA KIJIJI CHA MASAULWA WAKIONGOZWA NA DIWANI WA KATA HIYO BWANA ENOCK KISWAGA ALIYEVAA BARAGHASHIA KATIKATI YA MEZA KUU.
MWENYEKITI WA KIJIJI CHA MASAULWA BWANA ELIASY MGAYA AKIKILI KOSA LA KUMPA MUWEKEZAJI ENEO LA KIJIJI PASIPO WANANCHI NA HALMASHAURI YAKE YA KIJIJI KUTOFAHAMU JUU YA ENEO HILO.
KATIBU MWENEZI CCM KATA YA IMALINYI ANUEL NYADWIKE ANATOA SERA ZAKE KUHUSU UBINAFSISHAJI WA MAENEO KWA WAWEKEZAJI.
MASWALI YA WANANCHI WA KIJIJI CHA MASAULWA YAONEKANA KUWA YA JAZBA KUTOKANA NA KUUZWA KWA ENEO LA KIJIJI NA KUNYANG'ANYWA BAADHI YA MAENEO NA MUWEKEZAJI.
DIWANI KATA YA IMALINYI AKIZUNGUMZA NA WANANCHI JUU YA MUWEKEZAJI HUYO KUWA UONGOZI WA KIJIJI ULIKOSEA KUMPA MUWEKEZAJI ENEO LA KIJIJI PASIPO KUWASHIRIKISHA WANANCHI.
Diwani wa Kata ya Imalinyi Wilayani Wanging'ombe Mkoani Njombe Bw Enock Kiswaga Ameuagiza Uongozi wa Kijiji Cha Masaulwa Kumsimamishwa Mwekezaji wa Mashamba ya Kijiji Eneo la Idete Baada ya Kubaini Ukiukwaji Mkubwa wa Sheria za Kumpa Ardhi Mwekezaji Huyo.
Aidha Pia Diwani Huyo Ameuagiza Uongozi wa Kijiji Kuvunja Mkataba Uliosainiwa Kienyeji na Mwekezaji Huyo Kwani Tayari Umeanza Kuzua Malalamiko Kutoka Kwa Wananchi Baada ya Kuandika Barua Inayoonesha Kuwa Hawaridhishwi na Mchakato Mzima wa Kumpata Mwekezaji Huyo.
Akizungumza Wakati wa Mkutano wa Hadhara Uliofanyika Kijijini Humo Jana Bw Kiswaga Amesema Kuwa Kitendo Cha Serikali ya Kijiji Kusaini Mkataba na Mwekezaji Bila Kuwashirikisha Wananchi na Halmashauri ya Kijiji ni Hatari Kwani Kinaweza Kusababisha Uvunjifu wa Amani Endapo Wananchi Wataendelea Kutokuridhishwa na Mkataba Huo.
Wakizungumza Kwenye Mkutano Huo Baadhi ya Viongozi wa Kijiji Wanakiri Kutenda Kosa Hilo Kwa Kuingia Mkataba na Mwekezaji Bila Kuwashirikisha Wananchi na Hivyo Kuahidi Kuchukua Hatua Zitakazoridhiwa na Pande Zote
Eusebius Mtasiwa ni Kaimu Afisa Mtendaji wa Kijiji Hicho Pamoja Nae Elias Mgaya Mwenyekiti wa Kijiji Hicho Anawasilisha Ombi la Kuwaomba Wananchi Kuruhusu Angalau Mwekezaji Huyo Aendelee Kulima Kwa Miaka Mitano Ijayo Licha ya Kukiri Kosa Katika Uingiaji wa Mkataba Huo
Awali Wakizungumza Kwenye Mkutano Huo Wananchi Hao Wamesema Bado Kijiji Hicho Kimeendelea Kuwa na Kero Mbalimbali Zinazotokana na Uongozi wa Kijiji Kutawala Zaidi Kwa Kutumia Mabavu
Zaidi ya ekari 16 za eneo la Idete zimedaiwa kubinafsishwa kwa muwekezaji wa Igwachanya bwana Kilamlya bila kuwashirikisha wananchi hali ambayo imedaiwa na wananchi wa kijiji hicho kuwa wanahitaji ardhi yao na si vinginevyo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment