WAMILIKI NA MADEREVA WA BODABODA NA BAJAJI WAKIWA KWENYE MKUTANO WA KUREJESHWA KWA BAJAJI BARABARANI
MKUU WA MKOA WA NJOMBE CHRISTOPHA OLE SENDEKA AKIWASILI KATIKA UKUMBI WA TURBO MJINI NJOMBE KUWASIKILIZA KERO MADEREVA NA WAMILIKI WA PIKIPIKI ZA MAGURUDUMU MAWILI NA MATATU BAJAJI
TAZAMA MABANGO MBALIMBALI YA KERO HAPA CHINI NI KERO ZA BODABODA NA BAJAJI ZIKIWASILISHWA KWA MKUU WA MKOA WA NJOMBE.
NJOMBE
Hatimaye Sakata La Kuzuiliwa Kwa Bajaji Zisifanye Kazi Katika Barabara Kuu Limepatiwa Ufumbuzi Na Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Christopha Ole Sendeka Baada Ya Kuruhusu Bajaji Hizo Kuendelea Kufanya Kazi Kama Kawaida.
Ole Sendeka Pia Ameruhusu Wamiliki Wa Bajaji Na Wadau Wengine Wa Usafiri Kuongeza Bajaji Nyingine Arobaini Na Tano Ili Kufikisha Idadi Ya Bajaji 100 Tofauti Na Ilivyo Kwa Sasa Ambapo Bajaji 55 Pekee Ndizo Zinazofanya Kazi.
Bwana Sendeka Amesema Ofisi Yake Ipo Wazi Kuanzia Sasa Kwaajili Ya Kusikiliza Malalamiko Na Kero Za Madereva Bodaboda Na Bajaji Na Kuagiza Kuwa Asiwepo Kiongozi Yeyote Wa Kuwasumbua Kwa Kuwataka Wapaki Nje Ya Mji Siwepo Hali Hiyo.
Katika Hatua Nyingine Sendeka Ametumia Fursa Hiyo Kukemea Tabia Ya Kufanya Maandamano Yasiyo Rasmi Na Kusema Vijana Wasijaribu Kufanya Kazi Hiyo Kwani Serikali Haitalifumbia Macho Swala Hilo.
Awali Mwenyekiti Wa Bajaji Barnaba Mwangi Amesema Changamoto Kubwa Wanayokabiliwa Nayo Ni Kufukuzwa Kwenye Barabara Kuu Na Wanaosababisha Ni Wamiliki Wa Dalala Ambao Wanataka Wafanye Wao Biashara Ya Kusafirisha Abiria Huku Mwenyekiti Bodaboda Filemon Mwinuka Naye Akilia Na Tozo Mbalimbali Zinazotozwa.
Kwa Upande Wao Wamiliki Wa Bajaji Wakizungumza Kwa Fuaha Wamemshukuru Mkuu Wa Mkoa Kwa Juhudi Alizofanya Na Kusema Amejali Huduma Zinazotolewa Na Vyombo Hivyo Na Kutaka Viongozi Wengine Kuiga Mfano Huo.
No comments:
Post a Comment