MKUU WA MKOA WA NJOMBE CHRISTOPHA OLE SENDEKA AMESEMA WAMILIKI NA MADEREVA WA DALADALA WANATIKISHA KIBERITI KAMA KIMEJAA NA KUWAAMURU WARUDI BARABARANI KWA ATAKAYEGOMA ATAFUTIWA LESENI YA BIASHARA ZAKE ZOTE MKOA WA NJOMBE
KWA MSISITIZO MKUBWA WAKISIKILIZA HOJA ZA WAMILIKI ZA KWAMBA BAJAJI HAWAKO KISHERIA JAMBO AMBALO MKUU WA MKOA AMESEMA HATEGEMEI KUONDOA USAFIRI WA BAJAJI BARABARANI ISIPOKUWA KUONGEZA 45 ZIWE 100 DALADALA WAOMBA MSAMAHA ASIONGEZE NYINGINE .
WAMILIKI WA DALADALA MKOA WA NJOMBE WAKIWA KATIKA KIKAO NA MKUU WA MKOA WA NJOMBE CHRISTOPHA OLE SENDEKA BAADA YA KUGOMA KUFANYA KAZI MALALAMIKO YAO YAMESIKILIZWA LAKINI BADO MAAMUZI HAYAJACHUKULIWA HADI KAMATI ALIYOIUNDA MKUU WA MKOA IKUTANE NA ASIWEPO MTU WA KUFIKILIA KUZIONDOA BAJAJI BARABARANI.
MADEREVA DALADALA WAKITOKA NJE BAADA YA MKUU WA MKOA KUTOA MAAMUZI YAKE SASA WANATOKA KWENDA KUFANYA KIKAO CHAO CHA KURUDI BARABARANI.
NJOMBE
Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Christopha Olesendeka Amepiga Marufuku Kuwepo Kwa Migomo Ya Wamiliki Wa Usafiri Aina Yoyote Ile Kwamba Kwa Atakayebainika Kufanya Mgomo Atafutiwa Leseni Ya Biashara Yake.
Kauli Ya Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Olesendeka Imetolewa Kufuatia Wamiliki Wa Daladala mjini Njombe Kugoma Kusafirisha Abiria Kushinikiza Kuondolewa Kwa Usafiri Wa Pikipiki Za Magurudumu Matatu Maarufu Kama Bajaji Ambazo Zimeruhusiwa Kuendelea Kutoa Huduma Hivi Karibuni.
Olesendeka Amesema Kitendo Walichofanya Wamiliki Wa Magari Aina Ya Hice Cha Kugoma Kufanya Kazi Hajaridhishwa Nacho Nakwamba Atakayebaini Kuendekeza Migomo Na Maandamano Hatua Kali Zitachukuliwa Dhidi Yake Ikiwa Ni Pamoja Na Kufutiwa Leseni Za Biashara.
Baada Ya Mkuu Wa Mkoa Kusema Asiwepo Mtu Yeyote Atakaye Kuwa Na Mawazo Ya Kuziondoa Bajaji Barabarani Mwenyekiti Wa Wamiliki Wa Daladala Peter Haule Ameshukuru Kwa Maamuzi Na Kusema Wako Tayari Kufuata Utaratibu Utakao Kuwepo.
Nao Wamiliki Wa Daladala Walipopewa Nafasi Ya Kutoa Maoni Na Mapendekezo Yao Wamesema Bajaji Zinawamalizia Abiria Wote Walioko Mjini Ikiwa Wao Wanasafiri Umbari Mrefu Wa Kilomita 18 Kwa Shilingi Mia Nne Huku Bajaji Wanasafiri Umbali Wa Kilomita Tatu Kwa Shilingi Mia Tano .
Daladala Zimeamuliwa Kuendelea Na Kazi Hadi Mwafaka Wao Na Bajaji Na Bodaboda Utakapo Patikana Bila Kuwepo Mtu Wa Kushindwa Kufanya Kazi Ya Kutoa Huduma Ya Usafiri Kwa Abiria Katika Maeneo Yao.
No comments:
Post a Comment