Wafanyakazi wa TBL wakipata mafunzo sambamba na burudani za vinywaji baada ya saa za kazi.
Wafanyakazi wa TBL Mwanza wakifuatilia mafunzo ya mahusiano na afya.
TBL
Mbeya nao walishiriki mafunzo na mijadala ya mahusiano
Kampuni ya TBL Group chini ya kampuni mama ya ABInBev, imeitumia Siku
ya Wapendanao kuandaa semina za wafanyakazi wake kuhusiana na masuala
ya mahusiano katika familia, zilizoendeshwa na wataalamu wa masuala ya
Saikolojia na ushauri nasaha kutoka taasisi mbalimbali za mafunzo
nchini. Semina hizo zilifanyika katika viwanda vyake vilivyopo katika
mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Kilimanjaro na Arusha.
Kwa
kutumia kauli mbiu ya ‘Nogesha Upendo Valentine hii’ wafanyakazi
walipata fursa ya kupata mafunzo,na kushiriki mijadala kuhusiana na
mahusiano bora katika ndoa na familia sambamba na changamoto
mbalimbali zilizopo, pia waliweza kupata majibu na ushauri wa changamoto
hizo waliokuwa wakiendesha mafunzo.
No comments:
Post a Comment