MC AKITANGAZA UTARATIBU WAKATI WA WAGENI KUWASILI LUPEMBE
MBUNGE WA LUPEMBE AKIWA MGENI RASMI KWENYE KIKUNDI CHA WAPENDANAO KATIKA SIKU YA SHEREHE YA WAPENDANAO LUPEMBE
MGENI RASMI ANAKABIDHI CHEKI ZA WANAKIKUNDI
ZAWADI ZINAPELEKWA KWA WANAKIKUNDI ZA KUTOKA VIKUNDI JIRANI
Katika Vikundi Mbalimbali Vya Kuweka Na Kukopa Kwaajili Ya Kuinuana Kiuchumi Na Kuboresha Mfumo Wa Rishe Na Makazi Kwa Kujenga Nyumba Zenye Hadhi Zitakazojengwa Kwa Bati.
Akizungumza Na Wanakikundi Cha Wapendanao Kilichopo Lupembe Barazani Mbunge Wa Jimbo La Lupembe Joram Hongoli Amesema Wananchi Lazima Washiriki Kufanya Kazi Na Kuwahimiza Vijana Wa Kiume Kushirika Katika Kufanya Kazi Kwenye Maeneo Yao.
Bwana Hongoli Amezungumzia Pia Umuhimu Wa Utoaji Rishe Bora Kwa Watoto Kwaajili Ya Kukabiliana Na Tatizo La Udumavu Na Utapiamlo Kwamba Kila Mzazi Anapaswa Kuzingatia Kutoa Rishe Bora Kwa Watoto Wao Kwa Kuchanganya Vyakula Isiwe Vya Wanga Pekee.
Mwenyekiti Wa Kikundi Cha Wapendanao Cha Silc Lupembe Bi.Rehema Malekela Amesema Kikundi Hicho Chenye Washiriki 28 Kimefanikiwa Kukusanya Zaidi Ya Shilingi Milioni Kumi Kwa Mwaka Huku Risala Yao Iliyosomwa Na Brtazary Mveyange Ikitaja Changamoto Za Kukosa Viti.
Baadhi Ya Wanakikundi Wameshukuru Kwa Hamasa Iliyotolewa Na Afisa Maendeleo Ya Jamii Kata Kwani Vikundi Vingi Vya Akina Mama Vinaendesha Shughuli Zao Za Ujasiliamali Na Kuomba Serikali Kuwafikilia Kuwapatia Mikopo Pasipo Ubaguzi Wowote.
No comments:
Post a Comment