Naibu
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso, ameziagiza halmashauri zote
nchini kutowapa kazi za utekelezaji wa miradi ya maji wakandarasi
wasiojali maslahi ya taifa na kusisitiza kuwa Serikali haitavumilia
wakandarasi wazembe, ambao wanapewa kazi lakini wanashindwa kuzimaliza
kwa muda uliopangwa.
Aweso
alitoa agizo hilo wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya
Shinyanga na wakazi wa Kijiji cha Mendo, mkoani Shinyanga na
kusikitishwa na mwenendo wa utekelezaji usioridhisha wa mradi wa maji
kijijini hapo.
‘‘Nikuombe
sana Mkurugenzi wa Halmashauri, hakikisha mnawapa kazi wakandarasi
watakaohaikisha miradi inakamilika kulingana na mikataba yao, miradi
mingi ya Serikali imekua haina manufaa kwa wananchi na kukosa tija kwa
taifa kwa sababu tunawapa wakandarasi wazembe, wanaokosa uzalendo na
kutokujali maslahi ya taifa.’’
‘‘Mfano
mzuri ni mradi huu wa Mendo ulioanza kutekelezwa tangu Aprili 2014 na
ulitakiwa kukamilika Disemba 2017, lakini bado haujakamilika wakati
Serikali imeshaingia gharama ya zaidi ya Sh. mil 300. Jambo ambalo si
sahihi, hivyo naagiza ifikapo mwisho wa mwezi huu uwe umeshakamilika na
wananchi wapatao 2199 waanze kupata maji,’’ aliagiza Naibu Waziri Aweso.
Naibu
Waziri Aweso ameanza ziara ya siku 5 mkoani Sinyanga inayolenga kukagua
maendeleo ya miradi ya maji na kuweka msukumo katika utekelezaji wa
miradi hiyo kwa nia ya kuhakikisha inakamilika kwa wakati na wananchi
wa mkoa huo wanapata huduma ya maji ya uhakika kulingana na Ilani ya
Chama cha Mapinduzi.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akitembelea Kijiji cha Mendo, mkoani Shinyanga
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiongea na wananchi wa Kijiji cha Mendo, mkoani Shinyanga
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akikagua mtambo wa maji Kijiji cha Mendo, mkoani Shinyanga.
No comments:
Post a Comment