BWANA SETH YOHANA NI MKULIMA WA MATUNDA YA PARACHICHI NA TUFAA USALULE
HILI NI SHAMBA LA MATUNDA AINA YA TUFAA AUN APPLE YAKIWA SHAMBANI HAPA.
HAYA NI MAPARACHICHI AINA YA X IKULU AMBAYO YANATEGEMEWA KUVUNWA KUANZIA MWEZI FEBRUARY MWAKA HUU.
APPLE ILIYOSTAWI SHAMBANI HAPA BADO HAIJATOSHA KUCHUMWA
NJOMBE
Serikali Imeshauliwa Kuanzisha Banki Za Wakulima Katika Maeneo Mbalimbali Hapa Nchini Ili Kutoa Fursa Kwa Wakulima Kukopesha Mitaji Itakayosaidia Kuendesha Sekta Ya Kilimo Hususani Kwa Wenye Uwezo Mdogo Na Kukuza Uchumi Wa Nchi.
Rai Hiyo Imetolewa Na Baadhi Ya Wakulima Wa Kilimo Cha Parachichi Walioko Kijiji Cha Itipula Wakati Wakizungumza Na Uplands Fm Kuhusiana Na Changamoto Za Kilimo Hicho Ambapo Wamesema Baadhi Ya Wakulima Wanashindwa Kupewa Mikopo Kwenye Taasisi Za Kibenki Kwa Kuwa Kilimo Chao Ni Cha Muda Mrefu.
Aidha Wakulima Hao Akiwemo Seth Yohana Ambaye Ni Mkazi Wa Usalule Na Augustino Msigwa Aliyopo Kijiji Cha Itipula Wamesema Kuwa Kilimo Cha Parachichi Kinachangamoto Kubwa Ambazo Utatuzi Wake Unahitaji Mitaji Ambayo Wangepata Fursa Ya Kukopeshwa Na Benk Za Wakulima Ingesaidia Kilimo Kuwa Na Tija.
Wamesema Pia Watalaamu Wa Halmashauri Wanatakiwa Kuwatemelea Wakulima Vijijini Kusikiliza Kilio Chao Na Kutaka Serikali Kupitia Wizara Ya Kilimo Kuanzisha Benki Ya Kilimo Itakayo Mvumilia Mkulima Akikopa Arejesha Baada Ya Mavuno Ambayo Yanachukua Kuanzia Miezi Mitatu Na Kuendelea.
Kwa Upande Wake Mwenyekiti Wa Kamati Ya Mafunzo Na Uzarishaji Wa Kilimo Cha Parachichi Mkoa Wa Njombe Obed Mgaya Amesema Wakulima Bado Hawajaona Manufaa Ya Benki Za Wakulima Kwani Bado Hazijawafikia Wakulima Ambapo Kwa Sasa Wanashindwa Kukopa Kwenye Benk Nyingine Kutokana Na Kutoza Riba Kubwa.
Hata Hivyo Wakulima Wameshauriwa Kujikita Katika Kilimo Cha Matunda Mengine Aina Ya Tufaa au Apple Kwani Nayo Yanastawi Kwa Wingi Kati Wilaya Ya Wanging'ombe Kata Ya Ulembwe Mkoani Njombe.
No comments:
Post a Comment