MKUU WA WILAYA YA NJOMBE AKIONEKANA KUKASILISHWA NA KITENDO CHA KUTEKELEZA MAAGIZO YAKE KINYUME NA ALIVYOTARAJIA NJOMBE.
HAWA NI WAFANYABIASHARA WA MKOA WA NJOMBE WAKISIKILIZA MAJIBU YA MASWALI YAO NA KERO MBALIMBALI WALIZOZITOA KWA VIONGOZI WALIOKUWEPO KUSIKILIZA KERO ZAO LEO.
MEZA KUU IKIONGOZWA NA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA NJOMBE BWANA JASERY MWAMWALA AMBAYE AMEITISHA MKUTANO HUO KUSIKILIZA KERO ZA WAFANYABIASHARA IKIWA NI MIEZI MICHACHE TANGU ACHAGULIWE KUINGIA KWENYE UONGOZI WA CHAMA HICHO.
WAFANYABIASHARA WAKIWA NJE YA UKUMBI WA TURBO KUTOKANA NA UKUMBI HUO KUKOSA NAFASI NDANI.
MWENYEKITI WA JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA MKOA WA NJOMBE ONESMO MWAJOMBE AKIZUNGUMZA JUU YA KERO WANAZOKABILIANA NAZO IKIWEMO KUKADILIWA KODI NA TRA,PAMOJA NA KUKAA KWA MUDA MREFU WANAPOKWENDA KULIPA KODI ZA MAPATO YA BIASHARA ZAO.
HAPA MKUU WA WILAYA ANASEMA MIEZI MICHACHE ILIYOPITA ALIAGIZA KUWA WAFANYABIASHARA WANAOTEMBEZA BIDHAA AINA YA MATUNDA KWENYE MASINIA NA MIKOKOTENI, WANAOUZIA KWENYE MILANGO YA VIBANDA VYA NYUMBANI MWAO MALI MBICHI KAMA MATUNDA, NYANYA NA MBOGAMBOGA WANARUHUSIWA LAKINI ANASHANGAA MAAGIZO YAKE KWENDA TOFAUTI NA ALIVYOAGIZA, ANASEMA ALIMUAGIZA MKURUGENZI KWAMBA WANAOUZIA KWENYE NYUMBA ZAO,KUTEMBEZA WAENDELEE SASA KWANINI IMETOKEA TOFAUTI?
HUYU NI MWENYEKITI WA CCM MKOA WA NJOMBE JOSERY MWAMWALA AKITOA MAAGIZO KWA VIONGOZI WALIO CHINI YAKE WA CHAMA NA SERIKALI.
KULIA MWENYE KOTI LILILOKABA SHINGO NI BWANA MSANGO AMBAYE NI WAKALA WA KAMPUNI YA IHAGALA AUCTION MARK AMBAYE AMELALAMIKIWA MARA NYINGI NA WAFANYABIASHARA HAO KWAMBA OPARESHENI ANAZOFANYA ZINAKWENDA KINYUME NA UTARATIBU NA KANUNI KWANI ANAKAMATA WAFANYABIASHARA HATA SAA KUMI NA MBILI NA SAA MOJA USIKU.
NJOMBE
Mkuu Wa Wilaya Ya Njombe Bi. Luth Msafiri Amezitupia Lawama Halmashauri Zilizopo Katika Wilaya Ya Hiyo Kwa Kushindwa Kutekeleza Maagizo Yake Ambayo Wamekubaliana Kwenye Mikutano Na Kutekeleza Kinyume Na Maagizo Yake.
Bi.Msafiri Ametoa Kauli Hiyo Kufuatia Kupokea Malalamiko Kutoka Kwa Wafanyabiashara Mjini Njombe Wakilalamikia Kufanyika Kwa Oparesheni Za Kuwakamata Wanaouzia Bidhaa Zao Za Mbogamgoga Nyumbani Na Kutembeza Barabarani Kwamba Waliruhusiwa Lakini Anashangaa Wafanyabiashara Wadogo Kukamatwa Na Kudhalilishwa.
Bi.Msafiri Amesema Analaani Kitendo Kilichofanywa Na Kampuni Ya Ihagala Auction Mark Inayomilikiwa Na Msango Kwamba Haukuwa Wa Kibinadamu Kwani Ulikuwa Wa Kiudhalilishaji Na Unyanyasaji Kwa Wafanyabiashara Na Kutaka Mkurugenzi Kuzingatia Maagizo Yake Vizuri.
Katika Hatua Nyingine Bi.Msafiri Ametaka Watumishi Wa TRA Kutumia Rugha Zenye Staha Kwa Wafanyabiashara Na Kusema Hategemei Kuona Zinaendelea Katikia Wilaya Yake Huku Akisema TRA Mkoa Ni Jina Na Hivyo Wanapaswa Kuzingatia Maagizo Ya Mkuu Wa Wilaya.
Awali Wafanyabiashara Wamehoji Maswali Mbalimbali Ambayo Yamemfanya Mkuu Wa Wilaya Kusimama Na Kutoa Tamko Hilo Mbele Ya Mwenyekiti Wa CCM Mkoa Wa Njombe Jasely Mwamwala Yakiwemo Ya Kero Ya Kutozwa Kodi, Kukamatwa Kwa Wafanyabiashara Wadogo Bila Utaratibu Na TRA Kufanya Kazi Kwa Kuwakandamiza Wafanyabiashara.
Wamesema Mara Nyingi Wamekuwa wakienda ofisi za TRA Kulipa Kodi Ya Mapato Lakini Watendaji Wa Mamlaka Ya Mapato Tanzania Wilaya Ya Njombe Wamekuwa Hawawajali Na Kuwaona Kama Maadui Huku Huduma ZIkishindwa Kutolewa Kwa Wakati.
Pia Wafanyabiashara Hao Wamlalamikia Kuwepo Na Tatizo La Gari La Taka Kutochukua Taka Kwa Wakati Wakati Licha Ya Kutoa Fedha Shilingi Elfu Tatu Ambayo Bado Utaratibu Wake Haujawekwa Wazi Kwao.
Onesmo Mwajombe Ni Mwenyekiti Wa Jumuiya Ya Wafanyabiashara Mkoa Wa Njombe JWT Ambaye amesema Huduma Za TRA Hazitolewi Kikamilifu Kutokana Na Mtazamo Hasi Wa Kutaka Kutengeneza Njia Za Kushawishi Kuwepo Na Vitendo Vya Rushwa Nakwamba Mfanyabiashara Akienda Ofisi Za TRA Kulipa Kodi Anaonekana Kama Mbaya Kwao Badala Ya Kuwapokea Vizuri.
Mwenyekiti Wa CCM Mkoa Wa Njombe Jasery Mwamwala Amesema Amepokea Kero Hizo Na Kumtaka Katibu Wa CCM Mkoa Wa Njombe Hosea Mpagike Kushirikiana Na Mkuu Wa Wilaya Kuhakikisha Wanazifanyia Kazi Kero Hizo Na Kumpatia Majibu Ili Ayapeleke Kwa Wafanyabiashara Hao Ifikapo January 29.
No comments:
Post a Comment