Mkaguzi
Msaidizi wa Uhamiaji, Hassan A. Ramadhan (kulia) akifafanua jambo kwa
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu (wa pili kulia) kuhusu
mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano inavyosaidia kurahisisha
mawasiliano na utendajikazi katika Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini
Pemba. Kamishna Sururu akiendelea na ziara ya kikazi, Mkoa wa Kusini
Pemba tarehe 18 – 19 Disemba, 2017.
Mkaguzi
Msaidizi wa Uhamiaji, Juma A. Khamis (aliesimama) akichangia hoja
kwenye kikao cha Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu (hayupo
pichani) na Watumishi wa Idara ya Uhamiaji walioko Mkoa wa Kusini Pemba
leo tarehe 19 Disemba, 2017. Alisema “Ongezeko la Bandari Bubu ndani ya
Wilaya ya Mkoani ni changamoto kubwa katika utekelezaji wa majukumu
yetu. Tunazo takriban Bandari bubu 103, tunaomba Idara itupatie gari la
kufanyia doria katika maeneo hayo”. Kwa upande wake Kamishna Sururu
katika ziara yake hiyo ya kikazi Mkoani humo, aliahidi kulifanyia kazi
ombi mapema iwezekanavyo.
Kamishna
wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu (kushoto) akikagua baadhi ya
magari chakavu yaliyopo katika Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Pemba,
yanayosubiri kupigwa mnada baada ya kukamilika kwa taratibu za uuzaji wa
Mali za Serikali. Wakati wa ziara ya kikazi Mkoa wa Kusini Pemba tarehe
18 – 19 Disemba, 2017. Pamoja na kutembelea maeneo mbali mbali ya
utendaji kazi Mkoani humo ikiwemo Bandari ya Mkoani, Bandari ya Wesha
iliyopo Chake Chake na Bandari bubu kadhaa. Kulia kwake ni Afisa
Uhamiaji Mkoa wa Kusini Pemba, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Abdi
Bulushi.
Kamishna
wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu akikagua kitabu cha utoaji wa
Hati za Dharura za Kusafiria “ETD” katika Ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya
Mkoani, zinazotolewa kwa Watanzania wanaohitaji kusafiri nje ya Nchi.
Huku akiwasisitiza Maofisa Uhamiaji katika utoaji wa Hati hizo
wazingatie vyema Sheria na Taratibu zilizopo ili kuepusha matumizi
yasiyo sahihi. Aliyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kikazi Mkoa wa
Kusini Pemba tarehe 18 – 19 Disemba, 2017. Hati za Kusafiria za Dharura
ni miongoni mwa Hati mbali mbali za Kusafiria zinazotelewa na Idara ya
Uhamiaji Nchini
Kamishna
wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu akiambatana na Maofisa
waandamizi wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar kukagua baadhi ya bandari Bubu
zinazotumiwa na wakaazi wa Shehia za Kengeja na Muwambe, Kusini
Magharibi mwa kisiwa cha Pemba, kwa shughuli mbali mbali za kiuchumi na
kijamii, ambazo hutumika kama vipenyo kwa watu kuingia na kutoka
visiwani humo kinyume na taratibu za Uhamiaji. Wakati alipofanya ziara
ya kikazi maeneo mbali mbali ndani ya Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini
Pemba tarehe 18 Disemba, 2017.
Kamishna
wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu akitoa nasaha zake kwa Maafisa,
Askari na watumishi Raia wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Pemba,
wakati akihitimisha ziara ya kikazi Mkoani humo Leo tarehe 19 Disemba,
2017. Aidha, Kamishna Sururu aliwataka watumishi wote kuzingatia maadili
ya kazi, pamoja na kutilia mkazo matumizi sahihi ya mitandao ya
kijamii. “Naelewa tupo kwenye utandawazi, lakini narudia kuwasihi
matumizi ya Mitandao ya kijamii itumike kwa kuzingatia Kanuni na
Miongozo ya Serikali, pia mjiepushe na utoaji wa Siri na Taarifa za
serikali, ni mwiko kutoa taarifa yoyote. fuateni Sheria na Taratibu
tulizowekewa”.
Kamishna
wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu akiambatana na Maofisa
waandamizi wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar kukagua baadhi ya bandari Bubu
zinazotumiwa na wakaazi wa Shehia za Kengeja na Muwambe, Kusini
Magharibi mwa kisiwa cha Pemba, kwa shughuli mbali mbali za kiuchumi na
kijamii, ambazo hutumika kama vipenyo kwa watu kuingia na kutoka
visiwani humo kinyume na taratibu za Uhamiaji. Wakati alipofanya ziara
ya kikazi maeneo mbali mbali ndani ya Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini
Pemba tarehe 18 Disemba, 2017.
Kamishna
wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu akiambatana na Maofisa
waandamizi wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar kukagua baadhi ya bandari Bubu
zinazotumiwa na wakaazi wa Shehia za Kengeja na Muwambe, Kusini
Magharibi mwa kisiwa cha Pemba, kwa shughuli mbali mbali za kiuchumi na
kijamii, ambazo hutumika kama vipenyo kwa watu kuingia na kutoka
visiwani humo kinyume na taratibu za Uhamiaji. Wakati alipofanya ziara
ya kikazi maeneo mbali mbali ndani ya Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini
Pemba tarehe 18 Disemba, 2017.
Afisa
Uhamiaji Mkoa wa Kusini Pemba, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Abdi Bulushi
akimuonesha Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu (wa pili
kulia) na Maafisa Uhamiaji aliombatana nao, matunzo na usafi wa
mazingira katika nyumba za Makaazi ya Askari wa Uhamiaji, zilizoko eneo
la Ndugukitu, Wilaya ya Chake chake, Mkoa wa Kusini Pemba. Kamishna
Sururu yupo Mkoa wa Kusini Pemba kwa ziara ya kikazi kuanzia tarehe 18 –
19 Disemba, 2018. Aidha, Nyumba hizo zilifunguliwa rasmi na Mhe. Makamo
wa Pili wa Rais, Balozi Seif Iddi mapema mwezi Januari, 2017.
Mojawapo
ya nyumba za Makaazi ya Askari wa Uhamiaji, zilizoko eneo la Ndugukitu,
Wilaya ya Chake chake, Mkoa wa Kusini Pemba. Kamishna Sururu yupo Mkoa
wa Kusini Pemba kwa ziara ya kikazi kuanzia tarehe 18 – 19 Disemba,
2018. Aidha, Nyumba hizo zilifunguliwa rasmi na Mhe. Makamo wa Pili wa
Rais, Balozi Seif Iddi mapema mwezi Januari, 2017.
No comments:
Post a Comment