MBUNGE VITI MAALUM MKOA NJOMBE KUPITIA CHADEMA LUCIA MLOWE AKIHOJI JUU YA WATU WALIOONDOLEWA ENEO LA UJENZI WA SOKO LA KIMATAIFA MAKAMBAKO KWAMBA HAWAJALIPWA FIDIA ZAO KWENYE MAENEO HAYO.
DODOMA
Serikali Imechukua Hatua Mbalimbali Ikiweno Uandaaji Wa Mipango Kabambe Itakayotumika Kuongoza , Kusimamia Na Kudhibiti Uendelezaji Wa Miji Pamoja Na Urasmishaji Wa Makazi Yasiyopangwa katika Maeneo Mbalimbali Nchini.
Waziri Wa Ardhi, Nyumba Na Maendeleo Ya Makazi Angelina Mabula Amesema Hayo Wakati Akijibu Swali La Mbunge Wa Viti Maalumu Mkoa Wa Njombe Kupitia CHADEMA Lucia Mlowe Aliyetaka Kujua Namna Serikali Ilivyojiandaa Kuondoa Msongamano Wa Magali Na Ujenzi Holela Unaotokana Na Udhaifu wa Upangaji Matumizi Bora Ya Ardhi .
Waziri Mabula Amesema Jukumu La Upangaji Wa Miji Lipo Chini Ya Mamlaka Za Upangaji Wa Miji Ambazo Ni Halmashauri Za Majiji, Miji , Manispaa ,Wilaya Na Mamlaka Za Miji Midogo Ambapo Hiyo ni Kwa Mujibu Wa Kifungu Naba 7 Kifungu Kidogo Cha Kwanza Cha Sheria Ya Mipango Miji Namba Nane Ya Mwaka 2007 Kinaelekeza Jukumu La Upangaji Na Uendelezaji Miji Ni La Mamlaka Hizo.
Waziri Huyo Amesena Hadi Kufikia Oct; 20 Mwaka 2017 Maandalizi Ya Mipango Kabambe Ya Miji 29 Ilikuwa Imefikia Katika Hatua Mbalimbali Ambapo Kati Ya Maeneo Hayo Ni Dar Es Salaamu,Iringa ,Arusha , Tanga Na Miji Midogo Ni Mafinga Na Njombe Ambapo Uandaaji Huo Unapangwa Na Serikali Kwa Kushirikiana Na Kampuni Za Upangaji .
Awali Mbunge Wa Viti Maalumu Mkoa Wa Njombe Bi.Lucia Mlowe Ameuliza Swali Kuwa Wananchi Wamekuwa Wakiondolewa Kwenye Makazi Yao Ikiwa Wakati Wanajenga Serikali Ilikuwa Inawaona Pasipo Kufanya Chochote Juu Ya Maeneo Wanayoyaendeleza Na Kuwasababishia Hasara Baadaye Huku Wabunge Wengine Wakihoji Kutopimwa maeneo Ya Taasisi Za Serikali Kama Shule, Hospitali Na Ofisi.
No comments:
Post a Comment