Daktari
bingwa wa upasuaji wa Hospitali ya Agakhan, Dkt Aidan Njau (kushoto)
akizungumza na waandishi wa habari juu ya huduma ya Upandikizaji wa
Matiti kwa wanawake waliokatwa matiti kutokana na majanga mbalimbali
ikiwemo karatani ya matiti kulia ni daktari bingwa wa upasuaji kutoka
hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt Edwin Mrema.
Dkt Edwin akiwa na baadhi ya wataalam wa magonjwa mbalimbali ya upasuaji.
Hospitali
ya Aga Khan imeanza kutoa bure huduma ya kupandikiza matiti kwa akina
mama waliopatwa na magonjwa mbalimbali yaliyowapelekea kukatwa kwa
kiungo hicho muhimu, ikiwemo wale waliokatwa kutokana na magonjwa ya
Kansa, ukatili na kuungua moto.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo hii Jijini Dar es Salaam, Daktari bingwa wa
kitengo cha upasuaji katika hospitali ya Aga Khan, Dr. Aidan Njau
amesema huduma iliyoanza leo ni kuhudumia mgonjwa mmoja mmoja ili
kusaidia wanawake wengi wenye matatizo hayo ambao wamekuwa wakiishi na
maumivu makali hata kujisikia vibaya katika jamii .
“Kwa
kuanzia tunaanza na wale wanawake waliokatwa matiti yao, tutatoa nyama
kwenye sehemu yake ya mwili na kuipandikiza kwenye sehemu iliyokatwa na
kuufanya muonekano wake urudi kama ulivyokuwa" amesema Dk. Njau.
Amesema
huduma hiyo, itawafanya watanzania kushuhudia wanawake wakipandikizwa
matiti jambo ambalo halijawahi kutokea hapa nchini na kuwaasa wanawake
wenye matatizo hayo wajitokeze hospitalini hapo kwa wingi kwa ajili ya
kupatiwa huduma hii ya bure.
Amesema,
upasuaji huo utafanywa na madaktari wawili ambao ni Daktari bingwa wa
kitengo cha upasuaji katika hospitali ya Aga Khan, Dr. Aidan Njau na
Daktari bingwa Edwin Mrema kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili wote
wakiwa na lengo la kurudisha furaha kwa wanawake wenye matatizo haya
waliyokwisha ipoteza.


No comments:
Post a Comment