KIKOSI cha timu ya Mbeya City kesho kinashuka dimbani kuvaana na timu ya Azam katika uwanja wa Azam Complex Chamazi kwa ajili ya mchezo wao wa kesho wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
Kuelekea
mchezo huo,Meneja wa Mbeya City , Geoffrey Katepa amesema kwamba wapo
hapa tangu juzi na wamekuwa wakifanya mazoezi yao Uwanja wa Uhuru na
wakiwa wameweka kambi katika hostel za wokovu maeneo ya kurasini.
“Leo
tumefanya mazoezi yetu ya mwisho hapa Uwanja wa Uhuru kujiandaa na
mchezo wetu wa kesho dhidi ya wenyeji wetu, Azam, dhamira kuu ikiwa ni
kutopoteza tena mechi,”amesema.
Katepa
amesema anafahamu mchezo huo utakuwa mgumu kwa sababu Azam watakuwa
wanacheza nyumbani kwao, lakini watapigana kiume kuhakikisha wanawazima
hapo hapo Azam Complex.
“Niseme
tu kwamba tunawaheshimu wapinzani wetu, ni timu nzuri na ina wachezaji
wazuri na walimu wazuri. Lakini hata sisi tuna wachezaji wazuri na
walimu wazuri na pia ni timu nzuri na ndio maana tupo kwenye nafasi
nzuri katika msimamo wa Ligi Kuu,”.
Amesema katika mchezo huo anaamini utakuwa mgumu sana kwa pande zote na kwa sasaMbeya
City inashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi
11 baada ya kucheza mechi saba, ikizidiwa pointi moja na Singida United
iliyo nafasi ya tano na inazidiwa pointi mbili na Azam FC iliyo nafasi
ya nne.
Simba,
Yanga na Mtibwa Sugar zote zinafungana kileleni mwa Ligi Kuu kwa kila
timu kuwa na pointi 15 baada ya kucheza mechi sana pia.
Mechi
nyingine za Ligi Kuu zinatarajiwa kuchezwa Jumamosi, mabingwa watetezi,
Yanga watamenyana na Simba, Uwanja wa Uhuru, Maji Maji wataikaribisha
Mwadui FC Uwanja wa Maji Maji mjini Songea, Mtibwa Sugar wataikaribisha
Singida United Uwanja wa Manungu, Turiani mjini Morogoro, Lipuli
watakuwa wenyeji wa Mbao FC Uwanja wa Samora mjini Iringa na Kagera
Sugar wataikaribisha Ndanda FC Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

No comments:
Post a Comment